-
HAMAS: Wananchi wa Palestina wanataka kukomeshwa kikamilifu uvamizi wa utawala wa Kizayuni
Dec 26, 2023 02:40Izzat al-Rishq, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS amesema: wananchi wa Palestina wanataka kukomeshwa na kuhitimishwa uvamizi wa maghasibu wa Kizayuni na si usitishaji vita wa muda ambapo baada ya muda fulani uvamizi na vitendo vya kigaidi vya maghasibu hao vinaanza kwa mara nyingine tena.
-
UN: Wanawake wawili Wapalestina wanauawa kila saa katika vita vya Israel dhidi ya Gaza
Dec 25, 2023 23:20Wanawake wawili wa Kipalestina wanauawa kila saa moja katika Ukanda wa Gaza katika vita vya maangamizi ya umati vya utawala wa Israel dhidi ya eneo hilo lililozingirwa.
-
Yemen yaionya Marekani kwamba Bahari ya Sham itakuwa 'uwanja wa vita unaoteketea'
Dec 25, 2023 23:18Yemen imeonya kuwa Bahari ya Sham (Bahari Nyekundu) itakuwa "uwanja wa vita unaoteketea" ikiwa Marekani na washirika wake watashikamana na "tabia yao ya uchokozi" na kuchochea mvutano katika njia ya kimkakati ya baharini.
-
Balozi wa Iran: Ulaya ichukue hatua za maana kukomesha mauaji ya kimbari Gaza
Dec 25, 2023 07:12Balozi wa Iran nchini Iraq amesema nchi za Ulaya zinapasa kuchukua hatua za maana kwa ajili ya kukomesha jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Changamoto zinazoikabili Israel na Marekani za kuendeleza vita vya Gaza
Dec 25, 2023 07:03Katika siku ya 80 ya uvamizi ulioanzishwa na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya Gaza, maafa makubwa linayopata jeshi la utawala huo dhalimu katika vita vya ardhini pamoja na mashambulio makali na makubwa linayofanya jeshi hilo katika maeneo mbalimbali ya Gaza, ni matukio ambayo yangali yanaendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.
-
Kukamatwa majasusi wa utawala wa Kizayuni na Wanamuqawama
Dec 25, 2023 02:37Makamanda wa muqawama wamewatia mbaroni majasusi wa utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza baada ya kuchunguza nyaraka za usalama zilizopatikana wakati wa operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa.
-
Hamas yasema Biden ni 'mshirika katika uhalifu' wa Israel dhidi ya Wapalestina
Dec 24, 2023 08:24Rais wa Marekani Joe Biden ni mshirika katika uhalifu wa mauaji ya kimbari inayaotekelezwa na waziri mkuu wa utawala haramu Israel Benjamin Netanyahu dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, afisa wa ngazi ya juu wa Hamas amesema.
-
Israel imegeuza Gaza kuwa Kaburi la Umati la Raia, yapuuza maazimio ya UN
Dec 24, 2023 07:51Palestina imeutuhumu utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kujaribu kuzuia utekelezaji wa azimio nambari 2720 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kufikishwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
-
Kambi za jeshi la Marekani zalengwa kwa makombora kaskazini mashariki mwa Syria
Dec 24, 2023 07:45Kambi mbili za jeshi vamizi la Marekani nchini Syria zimeripotiwa kushambuliwa katika mkoa wa Hasaka, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
-
Wanajeshi 8 wa Israel waangamizwa Gaza, 44 wajeruhiwa, 10 hali mahututi
Dec 24, 2023 03:27Neil Hagari, Msemaji wa Jeshi la utawala haramu wa Israel alitangaza jana Jumamosi kuhusu kuangamizwa askari 5 wa utawala huo na kujeruhiwa wengine 5 katika mapigano ya nchi kavu kati ya askari hao vamizi na Wanamuqawama wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.