Kukamatwa majasusi wa utawala wa Kizayuni na Wanamuqawama
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i106394-kukamatwa_majasusi_wa_utawala_wa_kizayuni_na_wanamuqawama
Makamanda wa muqawama wamewatia mbaroni majasusi wa utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza baada ya kuchunguza nyaraka za usalama zilizopatikana wakati wa operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa.
(last modified 2023-12-25T02:37:19+00:00 )
Dec 25, 2023 02:37 UTC
  • Kukamatwa majasusi wa utawala wa Kizayuni na Wanamuqawama

Makamanda wa muqawama wamewatia mbaroni majasusi wa utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza baada ya kuchunguza nyaraka za usalama zilizopatikana wakati wa operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa.

Kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Palestina, kitengo kimoja cha idara ya usalama ya muqawama wa Palestina kimetangaza kuwa makamanda wa muqawama walipata nyaraka za kistratijia zinazojumuisha taarifa nyeti za kiusalama kuhusu jinsi shirika la usalama wa ndani la utawala wa Kizayuni (Shabak) linavyowasiliana na majasusi wake katika Ukanda wa Gaza na jinsi majasusi hao wanavyofanya ujasusi kwa maslahi ya Wazayuni.

Ripoti hiyo imeeleza kwamba suala hilo ndilo lilisababisha harakati za Shirika la Kijasusi la Kizayuni huko Gaza kukabiliwa na matatizo makubwa katika mashambulizi ya Wazayuni katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utawala wa Kizayuni ambao ulianzisha hujuma ya kikatili ya Gaza kwa lengo la kuyaangamiza makundi ya muqawama wa Palestina ikiwemo Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) na kwa lengo la kuwakomboa mateka wake, haujaweza kufikia malengo yake hayo hata baada ya kupita wiki kadhaa za jinai zake katika eneo hilo, na badala yake kuamua kuzungumza na makundi hao ya Kipalestina.

Pamoja na hayo kujitakia makubwa Tel Aviv katika mazungumzo ya kubadilishana mateka kumepelekea kufeli mara kadhaa mwenendo huo na hivyo kuanzisha tena jinai zake za kinyama dhidi ya raia wasio na hatia huko Gaza.

Ijumaa asubuhi tarehe 1 Desemba na baada ya kumalizika muda wa usitishaji vita wa muda huko Gaza, jeshi katili la Kizayuni lilianza tena kulipua kwa mabomu ya ukanda wa Gaza, ambapo kufikia sasa zaidi ya Wapalestina 20,400,000 wameuawa shahidi na wengine zaidi ya 54,000 kujeruhiwa.