-
Jeshi la Israel lakiri: Zaidi ya Wazayuni 1,200 wameuawa
Oct 10, 2023 23:29Jeshi la utawala haramu wa Israel limeungama na kusema kuwa Wazayuni zaidi ya elfu moja na 200 wameangamizwa na wapiganaji wa makundi ya mapambano ya Palestina, tangu Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa ilipoanza Jumamosi iliyopita.
-
Ansarullah: Kimbunga cha al-Aqsa ni ushindi wa kihistoria
Oct 10, 2023 23:05Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amepongeza Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa na kueleza kuwa, shambulizi la kushtukiza la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina (HAMAS) na makundi mengine ya mapambano ya Palestina dhidi ya Israel ni ushindi wa kihistoria ambao umeleta mlingano wa nguvu na kuusabababishia hasara kubwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
UN: Kuiwekea Gaza mzingiro wa kila kitu ni 'marufuku' chini ya sheria za kimataifa
Oct 10, 2023 11:58Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema, mzingiro wa kila kitu ambao Israel imeamua kuuwekea Ukanda wa Gaza, na kuwanyima raia bidhaa muhimu kwa ajili ya maisha, umepigwa marufuku chini ya sheria za kimataifa.
-
Ayatullah Sistani: Waislamu wote wana wajibu wa kuwasaidia Wapalestina
Oct 10, 2023 10:39Kiongozi wa juu wa kidini wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq ametoa mwito kwa Waislamu kote duniani kuwaunga mkono, kuwahami na kuwasaidia wananchi wa Palestina, wakati huu ambapo utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kufanya mashambulizi ya kikatili dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.
-
Ulipizaji kisasi cha ushindi wa Kimbunga cha Al-Aqsa kwa raia na watoto wa Palestina
Oct 10, 2023 05:51Baada ya kushindwa na operesheni ya kimbunga cha Al-Aqsa, utawala wa Kizayuni kwa mara nyingine tena umezidisha mashambulizi yake ya anga katika maeneo ya makazi huko Ghaza, ambapo unajaribu kubadilisha mlingano wa vifo kwa manufaa yake.
-
Saraya al-Quds: Kama Israel inataka uhai wa wanajeshi waliotekwa nyara, iache kushambulia raia
Oct 10, 2023 03:42Saraya al-Quds, tawi la kijeshi la Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina ameuonya utawala ghasibu wa Israel na kuutaka uache mara moja kushambulia na kuua raia wasio na hatia kama inathamini uhai wa wanajeshi wake na walowezi wa Kizayuni wanaoshikiliwa mateka.
-
Jeshi la Israel laua hata mateka wa Kizayuni Ukanda wa Ghaza
Oct 09, 2023 23:07Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesitna HAMAS limetangaza kuwa, mateka wanne wa Kizayuni waliokuwa mikononi mwa wanamapambano wa Palestina wameuliwa katika mashambulio ya kiholela ya jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Mapambano yanaendelea kwa siku ya tatu, Hamas yapiga Ashkelon na Ashdod
Oct 09, 2023 11:33Mapigano kati ya wapigania ukombozi wa Palestina na jeshi la utawala vamizi wa Israel yameendelea leo kwa siku ya tatu katika maeneo ya ndani ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni karibu na Ukanda wa Gaza, ukiwa mwendelezo wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoanzishwa na Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Hamas) dhidi ya uvamizi wa Israeli, huku kukiwa na makadirio kwamba Wazayuni wasiopunguau 1,000 wa Israeli wameangamizwa hadi sasa.
-
Hatua za kichochezi za Marekani kuunga mkono utawala wa Kizayuni
Oct 09, 2023 06:16Kufuatia mashambulizi makubwa ya makundi ya mapambano na ukumbozi wa Palestina katika maeneo yanayouzunguka Ukanda wa Ghaza, ambayo yamedhihirisha udhaifu na utepetevu mkubwa wa utawala wa Kizayuni, Marekani imepanga na kutekeleza hatua za kichochezi kwa kisingizio cha eti kuiunga mkono Tel Aviv na kuimarisha ari ya Wazayuni.
-
Undani wa oparesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa kwa upande wa kijeshi na kiitelijinsia
Oct 09, 2023 04:43Makundi ya muqawama ya Palestina yenye makao katika Ukanda wa Ghaza yaani harakati ya Hamas na harakati nyingine za Palestina khususan Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina juzi Jumamosi tarehe 7 Oktoba yalianzisha oparesheni kwa jina la Kimbunga cha Al Aqsa dhidi ya utawala wa Kizayuni; oparesheni iliyouduwaza kikamilifu utawala huo na kuwashtua pakubwa Wazayuni.