Jeshi la Israel laua hata mateka wa Kizayuni Ukanda wa Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103276-jeshi_la_israel_laua_hata_mateka_wa_kizayuni_ukanda_wa_ghaza
Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesitna HAMAS limetangaza kuwa, mateka wanne wa Kizayuni waliokuwa mikononi mwa wanamapambano wa Palestina wameuliwa katika mashambulio ya kiholela ya jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 09, 2023 23:07 UTC
  • Jeshi la Israel laua hata mateka wa Kizayuni Ukanda wa Ghaza

Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesitna HAMAS limetangaza kuwa, mateka wanne wa Kizayuni waliokuwa mikononi mwa wanamapambano wa Palestina wameuliwa katika mashambulio ya kiholela ya jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, Abu Ubaidah, Msemaji wa Brigedi za Izzuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la HAMAS ametangaza habari hiyo na kusema kuwa, Wazayuni hao wanne waliuliwa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni katika mashambulizi ya usiku wa kuamkia jana Jumatatu.

Amesema kuwa, Wapalestina waliokuwa wanawalinda mateka hao nao wameuawa shahidi kwenye mashambulizi hayo ya kikatili ya wanajeshi wa Israel. 

Hadi hivi sasa hakujatangazwa idadi halisi ya mateka Wazayuni walioko mikononi mwa wanamapambano wa Palestina huku baadhi yao wakikadiria kuwa wanafikia 253. 

Wanajeshi Wazayuni wanafanya mashambulio ya kiholela Ghaza

 

Kabla ya hapo Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS liliuonya utawala wa Kizayuni kuwa, linawashikilia mateka Wazayuni wasio na idadi na limewaweka kwenye kona mbalimbali za Ukanda wa Ghaza, hivyo mashambulio ya kiholela ya Israel yatapelekea kuuawa Wazayuni wenzao. 

Mapigano kati ya wapigania ukombozi wa Palestina na jeshi la utawala vamizi wa Israel yanaendelea kwa siku ya nne mfululizo kwenye maeneo ya ndani ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni karibu na Ukanda wa Gaza, ukiwa mwendelezo wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoanzishwa na Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (HAMAS) dhidi ya uvamizi wa Israeli. Hadi tunaandaa ripoti hii, Wazayuni wasiopunguau 1,000 wa likukwa wameshaangamizwa na mamia ya wengine kujeruhiwa, huku idadi isiyojulikana wakiwa wametekwa na wanamapambano wa Palestina.