Jeshi la Israel lakiri: Zaidi ya Wazayuni 1,200 wameuawa
(last modified Wed, 11 Oct 2023 02:59:44 GMT )
Oct 11, 2023 02:59 UTC
  • Jeshi la Israel lakiri: Zaidi ya Wazayuni 1,200 wameuawa

Jeshi la utawala haramu wa Israel limeungama na kusema kuwa Wazayuni zaidi ya elfu moja na 200 wameangamizwa na wapiganaji wa makundi ya mapambano ya Palestina, tangu Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa ilipoanza Jumamosi iliyopita.

Brigedia Jenerali Dan Goldfus, Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) amekiri hayo mbele ya waandishi wa habari, na huku akilengwalengwa na machozi amesema kuwa, "Siku nne zilizopita zimekuwa nzito sana kwetu."

Kamanda huyo wa jeshi katili la utawala ghasibu wa Israel ameedelea kueleza kuwa, "Kwa bahati mbaya, mara hii wamefanikiwa kuua watu zaidi ya 1,000. Huwezi hata kusawiri."

Hata hivyo kamanda huyo mkuu wa jeshi la utawala wa Kizayuni hajatoa maelezo kuhusu idadi ya raia wa kigeni walioangamizwa katika operesheni ya makundi ya muqawama ya Palestina.

Aidha vyombo vya habari vya Kizayuni vimetangaza kuwa, Wazayuni zaidi ya 1,200 wameuawa na wengine 2,382 wamejeruhiwa, ambapo 345 miongoni mwao wako katika hali mahututi.

Wakati huo huo ndege za kivita za Israel zimeendelea kushambulia makazi ya raia katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza. Aghalabu ya wahanga wa hujuma hizo za kinyama za Israel ni wanawake na watoto wadogo.

Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu iliyoanza Jumamosi iliyopita, imengia siku yake ya tano leo.

Tags