-
Mkuu wa haki za binadamu wa UN ataka kusitishwa mpango wa Israel wa kuhalalisha kunyongwa Wapalestina
Jan 03, 2026 23:11Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Israel kusitisha mipango yake ya kutoa hukumu za kifo za lazima kwa Wapalestina na kutahadharisha kuwa pendekezo hilo linakiuka sheria za kimataifa.
-
Uhispania: Tuna wasiwasi kuhusu hali mbaya ya Gaza na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni Ukingo wa Magharibi
Jan 03, 2026 23:10Serikali ya Uhispania imeelezea wasiwasi mkubwa ilionao kuhusiana na hali mbaya ya Gaza na muendelezo wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Watoto wa Gaza walilipa gharama kubwa mwaka uliomalizika majuzi wa 2025
Jan 03, 2026 08:34Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watoto wa Gaza walilipa gharama kubwa mwaka uliomalizika wa 2025 kutokana na vita na mzingiro wa utawala wa Israel dhidi ya Ukanda huo.
-
Nchi za Waislamu zataka kuruhusiwa misaada ya kibinadamu Gaza
Jan 03, 2026 02:42Mawaziri wa Mambo ya Nje wa mataifa manane ya Waislamu wameitaka jamii ya kimataifa kuishinikiza Israel, kama dola linalokalia kwa mabavu ardhi za Palestina, kuondoa mara moja vizingiti na vikwazo vya kuingia kwa misaada ya msingi na ya dharura katika Ukanda wa Gaza.
-
Al-Jazeera: Israel inajiandaa kuanzisha tena mashambulizi makali Gaza
Jan 02, 2026 23:07Waziri wa Vita wa Israel, Israel Katz ameliagiza jeshi la utawala huo haramu kujiandaa kurejea kwenye mapigano makali dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Ukanda wa Gaza, hayo yameripotiwa na kanali ya televisheni ya al-Jazeera ikinukuu gazeti la Kizayuni la The Jerusalem Post.
-
Jackie Chan amwaga machozi kuwalilia watoto wa Ghaza
Jan 02, 2026 03:27Jackie Chan, muigizaji maarufu wa Hollywood na filamu za Hong Kong, amewaga machozi kuwalilia watoto wa Ghaza akielezea huzuni yake kubwa kutokana na hali mbaya ya kibinadamu katika ukanda huo akitangaza kwamba alipotazama video ya mahojiano na mtoto wa Palestina alilia na kumkumbusha tena mateso yasiyoisha ya watoto wa Ghaza.
-
Fat’h: Hatua zozote za kikanda bila ya kutatua kadhia ya Palestina zitashindwa tu
Jan 02, 2026 03:24Mmoja wa viongozi waandamizi wa harakati ya ukombozi wa Palestina ya Fat’h amesema kuwa, Makubaliano ya Abraham ni udanganyifu wa kisiasa na hayatoleta utulivu katika eneo hili maadamu yanapuuza kadhia ya Palestina.
-
Baraza la Makanisa Duniani lataka kuwekewa vikwazo Israel kutokana na vita vya Gaza
Jan 01, 2026 23:18Baraza la Makanisa Duniani (WCC) limeutaka Umoja wa Ulaya (EU) kuiwekea Israel vikwazo vikiwemo vya silaha kutokana na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni huko Gaza, na ukiukaji wa haki dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.
-
Kwa nini kiwango cha kujiua katika jeshi la Israel kimefikia kiwango cha juu zaidi?
Jan 01, 2026 23:06Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Isarel, kwa kukiri kujiua kwa makumi ya wanajeshi wake, limekubali kuwa jumla ya wanajeshi 151 wamepoteza maisha katika mwaka huu wa sasa.
-
2025, mwaka mbaya zaidi kwa Wapalestina kufuatia mauaji ya kimbari ya Israel
Jan 01, 2026 08:51Ofisi Kuu ya Takwimu ya Palestina imeripoti kuwa mwaka 2025 ulikuwa mwaka mbaya zaidi katika uga wa kibinadamu na idadi ya jamii ya watu huko Palstina kutokana na vita vya Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na kuongezeka kwa ukiukaji wa sheria katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ikiwa ni pamoja na Quds Mashariki.