Jackie Chan amwaga machozi kuwalilia watoto wa Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i135026-jackie_chan_amwaga_machozi_kuwalilia_watoto_wa_ghaza
Jackie Chan, muigizaji maarufu wa Hollywood na filamu za Hong Kong, amewaga machozi kuwalilia watoto wa Ghaza akielezea huzuni yake kubwa kutokana na hali mbaya ya kibinadamu katika ukanda huo akitangaza kwamba alipotazama video ya mahojiano na mtoto wa Palestina alilia na kumkumbusha tena mateso yasiyoisha ya watoto wa Ghaza.
(last modified 2026-01-03T09:06:27+00:00 )
Jan 02, 2026 06:57 UTC
  • Jackie Chan amwaga machozi kuwalilia watoto wa Ghaza

Jackie Chan, muigizaji maarufu wa Hollywood na filamu za Hong Kong, amewaga machozi kuwalilia watoto wa Ghaza akielezea huzuni yake kubwa kutokana na hali mbaya ya kibinadamu katika ukanda huo akitangaza kwamba alipotazama video ya mahojiano na mtoto wa Palestina alilia na kumkumbusha tena mateso yasiyoisha ya watoto wa Ghaza.

Sambamba na siku ya kwanza ya Mwaka Mpya wa 2026, imeenea sana katika mitandao ya kijamii, video ya mwigizaji maarufu wa Hollywood na filamu ya Hong Kong, Jackie Chan, ambapo nyota huyo maarufu wa filamu anazungumzia athari mbaya ya vita kwa watoto na raia wa Ghaza.

Katika video hiyo, Jackie Chan anaeleza kwamba hivi majuzi aliona video ya mahojiano na mtoto wa Palestina huko Ghaza ambayo ilimuathiri sana. Katika mahojiano hayo, mtoto anapoulizwa: "Unataka kuwa nani utakapokuwa mkubwa?" Mtoto anajibu kwa kusema: "Watoto hawakui wakawa wakubwa katika eneo letu."

Maneno hayo machungu na kuhuzunisha mno ya mtoto huyo wa Ghaza yalimliza Jackie Chan na anasema kwenye mahojiano hayo kwamba: "Nilipoona video hii, nililia na machozi yangu yalitiririka bila ya kukoma." Jackie Chan ameongeza kuwa, watoto wa Ghaza wanaishi ndani ya mashambulizi ya mabomu kila siku na ukweli huu mchungu umewanyima dhana ya kufurahia utoto wao siseni tena mustakabali wao.

Jackie Chan amesisitiza pia kwamba mashambulizi ya kila siku yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza yanaukumbusha ulimwengu kwamba kufikia utu uzima kwa watoto wengi katika eneo hilo si haki yao ya kimsingi na ni ndoto isiyoweza kufikiwa. Ametaka maoni ya walio wengi duniani yazingatiwe kuhusu kukomeshwa mateso ya watoto na raia katika mgogoro mkubwa wa kibinadamu huko Ghaza.