-
Arab League: Jamii ya Kimataifa ikomeshe ukaliaji ardhi kwa mabavu unaofanywa na Israel
Mar 31, 2023 04:13Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeitaka Jamii ya kimataifa ichukue hatua za dhati kukomesha ukaliaji ardhi kwa mabavu unaofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Ansarullah yalaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu
Mar 30, 2023 22:41Harakati ya Ansarullah ya Yemen imelaani vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Denmark na katika nchi nyingine za Ulaya.
-
Waziri wa Ulinzi wa Yemeni: Muungano vamizi utajuta iwapo utaendeleza vita
Mar 30, 2023 08:37Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen ameuonya muungano wa Waarabu unaoongozwa na Saudi Arabia kwamba utajuta iwapo hautasikiliza mapendekezo ya Katibu Mkuu wa harakati ya Ansarullah kuhusu suala la kusimamisha mashambulizi dhidi ya watu wa Yemen.
-
OIC na Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu zalaani kuvunjiwa heshima msikiti wa al-Aqswa
Mar 30, 2023 04:13Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Kiislamu zimelaani vikali hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti mtakatifu wa al-Aqswa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Jihadul-Islami yatoa wito Wapalestina wote wazatitiwe kwa silaha kujibu mapigo kwa wazayuni
Mar 29, 2023 03:40Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imewasilisha kwa wawakilishi wa makundi mengine ya mapambano ya Palestina mpango wa kuwapa silaha Wapalestina wote ili kukabiliana na mpango wa Itamar Ben Guer, waziri wa usalama wa ndani wa utawala haramu wa Israel kuhusu kuwapatia silaha walowezi wa Kizayuni.
-
FAO: Mamilioni ya watu Afghanistan wako katika hatari ya njaa
Mar 28, 2023 22:41Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeonya kuhusu hatari ya njaa kwa mamilioni ya watu nchini Afghanistan.
-
Waandamanaji Israel waapa, maandamano yataendelea hadi ‘mageuzi ya mahakama’ yatakapofutiliwa mbali
Mar 28, 2023 22:40Kiongozi wa waandamanaji dhidi ya serikali ya utawala haramu wa Israel ameapa kuwa maandamano yataendelea katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu licha ya waziri mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu, kutangaza kuwa mpango tata wa marekebisho ya mahakama ya utawala huo umeakhirishwa hadi mwezi ujao.
-
Taliban: Waafghani ndio walengwa wakuu wa mashambulio ya DAESH (ISIS)
Mar 28, 2023 08:12Naibu Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Taliban anayehusika na masuala ya kisiasa amesema, wananchi wa Afghanistan ndio walengwa wakuu wa hujuma na mashambulio ya kundi la kigaidi la DAESH (ISIS).
-
Hizbullah: Ni kupoteza muda tu kuweka matarajio ya kumchagua rais kwa msaada kutoka nje
Mar 28, 2023 07:59Mjumbe wa baraza kuu la Hizbullah ya Lebanon amesema, kuweka matarajio ya kumchagua rais kwa msaada kutoka nje ni kupoteza muda tu katika wakati mgumu ilioko nchi hiyo hivi sasa.
-
HAMAS: Israel kuwafukuza waumini katika msikiti wa Al Aqsa ni sawa na kuanzisha vita vya kidini
Mar 28, 2023 07:54Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani kuondolewa kwa nguvu waumini wa Kiislamu katika eneo la Msikiti wa al-Aqsa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kutangaza vita vya kidini dhidi ya Wapalestina na ni jaribio la kubadilisha utambulisho wa Kiislamu wa eneo hilo takatifu.