Waziri wa Ulinzi wa Yemeni: Muungano vamizi utajuta iwapo utaendeleza vita
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i95702-waziri_wa_ulinzi_wa_yemeni_muungano_vamizi_utajuta_iwapo_utaendeleza_vita
Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen ameuonya muungano wa Waarabu unaoongozwa na Saudi Arabia kwamba utajuta iwapo hautasikiliza mapendekezo ya Katibu Mkuu wa harakati ya Ansarullah kuhusu suala la kusimamisha mashambulizi dhidi ya watu wa Yemen.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Mar 30, 2023 08:37 UTC
  • Meja Jenerali Mohammad Nasser Al-Atefi
    Meja Jenerali Mohammad Nasser Al-Atefi

Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen ameuonya muungano wa Waarabu unaoongozwa na Saudi Arabia kwamba utajuta iwapo hautasikiliza mapendekezo ya Katibu Mkuu wa harakati ya Ansarullah kuhusu suala la kusimamisha mashambulizi dhidi ya watu wa Yemen.

Abdul-Malik Badruldeen al-Houthi, Katibu Mkuu wa Ansarullah ya Yemen amezishauri Saudi Arabia na Imarati kuepuka kuingia katika mwelekeo wa kudhamini maslahi ya Marekani, na badala yake wajali maslahi yao, watekeleze makubaliano ya kubadilishana mateka na kuondoa mzingiro wa Yemen.

Al-Houthi amesema: "Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni wa Israel zinataka Saudi Arabia na Imarati ziendeleze vita vya Yemen. Njia pekee ya amani ni kukomesha mashambulizi na kuondoa mzingiro, kukomesha uvamizi, kuanza ujenzi, kutoa fidia za uharibifu wa vita na kukamilisha mchakato wa kubadilishana mateka wa vita. 

Kwa mujibu wa ripoti ya leo Alhamisi ya televisheni ya "Al-Masira, Meja Jenerali Mohammad Nasser Al-Atefi, Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen, amezionya nchi wavamizi na kusema: Sikilizeni mapendekezo ya Katibu Mkuu wa Ansarullah nchini Yemen ya kukomesha uchokozi, kuondoa mzingiro na kuondoka katika ardhi ya Yemen.

Al-Atefi amezitishia nchi za muungano wa Saudia kwamba vita vya baadaye vitakuwa vita vya uwezo, kammaliza kabisa adui na ushindi wa haki.