-
Uamuzi madhubuti wa bunge la Jordan wa kumfukuza balozi wa Israel.
Mar 24, 2023 03:45Mvutano umeibuka katika uhusiano wa Amman na Tel Aviv kufuatia uamuzi imara wa Bunge la Jordan wa kumfukuza balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini humo.
-
Marubani wa Israel wakataa kumpeleka Netanyahu Uingereza
Mar 24, 2023 03:35Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amelazimika kuakhirisha safari yake ya kuitembelea Uingereza, baada ya marubani kadhaa wa utawala huo kukataa kumsafirisha kwa ndege katika nchi hiyo ya Ulaya mtawala huyo mwenye misimamo mikali.
-
Ubaguzi wa rangi wa baraza la mawaziri la Netanyahu na hasira ya serikali ya Jordan
Mar 23, 2023 22:50Matamshi ya karibuni ya mmoja wa mawaziri wa baraza lenye misimamo ya kupindukia mipaka la Benhamini Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel yameikasirisha serikali ya Jordan. Misimamo mikali na ya ubaguzi wa rangi ya baraza hilo hadi sasa imeugharimu pakubwa utawala huo kieneo na kimataifa.
-
GCC: Mapatano ya Saudia, Iran kuhitimisha migogoro katika eneo
Mar 23, 2023 07:41Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (GCC) limepongeza makubaliano ya hivi karibuni kati ya Iran na Saudi Arabia ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia uliokuwa umevunjika kwa kipindi cha miaka saba.
-
Nasrullah: Uvamizi wa kijeshi wa Israel dhidi ya Lebanon utajibiwa haraka
Mar 23, 2023 07:33Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amepuuzilia mbali vitisho vilivyotolewa hivi karibuni na maafisa wa utawala haramu wa Israel vya kuwepo uwezekano wa kuivamia kijeshi Lebanon na kusisitiza kuwa, uchokozi wowote wa Israel dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu utapata jibu la haraka.
-
Kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kusini mwa Quds Tukufu
Mar 23, 2023 04:33Meya wa mji mtakatifu wa Quds ametoa idhini ya kujengwa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika mji huo, jambo ambalo linaenda kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Sana'a: Raia elfu 49 wameuawa na kujeruhiwa tangu kuanza vita hadi sasa
Mar 23, 2023 03:57Wizara ya Haki za Binadamu ya Yemen imetangaza kuwa hadi sasa raia elfu 49 wameuawa na kujeruhiwa tangu muungano vamizi dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudia uanzisha vita nchini humo mwaka 2015.
-
Mapatano ya Kiusalama kati ya Iran na Iraq; azma thabiti ya kukabiliana na vitisho
Mar 22, 2023 22:43Katika hafla iliyohudhuriwa na Mohammad Shia as-Sudani, Waziri Mkuu wa Iraq hapo siku ya Jumapili tarehe 19 Machi mwaka huu, makubaliano ya ushirikiano wa usalama wa pamoja wa kati ya nchi mbili jirani za Iran na Iraq yalitiwa saini na Admeri Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Kitaifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na Qasim al-Aarji, Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Waziri Mkuu wa Iraq.
-
Bunge la Jordan lapasisha pendekezo la kutimuliwa balozi wa Israel mjini Amman
Mar 22, 2023 09:04Wawakilishi wa Bunge la Jordan wamepigia kura ya ndio pendekezo la kufukuzwa balozi wa utawala haramu wa Israel huko Amman wakilalamikia na kupinga hatua ya waziri wa fedha katika serikali ya mrengo wa kulia ya Israel, ambaye alizua utata mapema wiki hii.
-
Umoja wa Mataifa: Msimamo wetu haujabadilika, tunapinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi
Mar 22, 2023 09:04Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, umoja huo unapinga kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel na kusisitiza kwamba, msimamo wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na kadhia hiyo haujabadilika.