-
Mwakilishi wa US adai vita vya Israel dhidi ya Lebanon haviepukiki ikiwa Hizbullah haitapokonywa silaha
Oct 20, 2025 06:10Tom Barrack, balozi wa Marekani nchini Uturuki na mjumbe maalumu wa masuala ya Syria, ametoa onyo la kutisha kwa Lebanon akiitaka ama iipokonye silaha Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya nchi hiyo Hizbulla au ikabiliwe na mashambulizi mengine ya Israel na migogoro ya kiuchumi na kisiasa.
-
Idara ya Vyombo vya Habari vya Serikali Gaza yasajili ukiukaji 80 wa Israel tangu kusitishwa mapigano
Oct 20, 2025 03:08Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali katika Ukanda wa Gaza imesema ukiukaji wa Israeli wa mapatano ya kusitisha vita unaakisi hamu ya utawaka huo vamizi ya kuzidisha machafuko na mtazamo wake wa kichokozi dhidi ya watu wa ukanda huo.
-
Ripoti: Asilimia 97 ya shule za Gaza zimeharibiwa kwa mashambulizi ya Israel
Oct 19, 2025 23:58Ripoti rasmi zinasema, mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel yameharibu asilimia 97 ya shule za Ukanda wa Gaza na hivyo kuhatarisha mustakbali wa kielimu wa wanafunzi laki tatu wa Kipalestina katika eneo hilo.
-
Hamas yakanusha madai ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ya kukiuka usitishaji mapigano
Oct 19, 2025 07:54Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imekanusha vikali madai yaliyomo katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwamba harakati hiyo imekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza.
-
Pakistan na Afghanistan zafikia makubaliano ya kusitisha mapigano
Oct 19, 2025 07:48Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza kuwa Pakistan na Afghanistan zimekubaliana kusitisha mapigano mara moja katika mazungumzo yaliyofanyika Doha.
-
Hizbullah: Vita vya utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya kusini mwa Lebanon vingali vinaendelea
Oct 18, 2025 23:13Mbunge mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon Hizbullah amesisitiza kuwa, vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya maeneo ya kusini mwa Lebanon vingali vinaendelea kwa malengo maalumu na kwa sura tofauti.
-
HAMAS: Hatutajifunga kukabidhi silaha mpaka yatakapofanyika mazungumzo zaidi
Oct 18, 2025 23:12Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza kuwa haitajifunga moja kwa moja kukabidhi silaha na inatumai usitishaji vita na utawala wa kizayuni wa Israel utadumu kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano ili kuijenga upya Ghaza.
-
ICC yatupilia mbali rufaa ya Israel dhidi ya hati za kutiwa nguvuni Netanyahu na Gallant
Oct 18, 2025 23:11Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imekataa ombi la utawala wa kizayuni wa Israel la kukata rufaa dhidi ya hati za kukamatwa waziri mkuu wake Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wa vita wa utawala huo ghasibu Yoav Gallant kuhusiana na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na jeshi la kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.
-
Umoja wa Mataifa: Kiwango cha uharibifu katika Ukanda wa Gaza hakitasawariki
Oct 18, 2025 09:25Tom Fletcher, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Misaada ya Kibinadamu, amesema kuwa, kiwango cha uharibifu katika Ukanda wa Gaza haikitasawariki kiasi kwamba, ni vigumu kuamini hali hiyo kwani kila kitu kimeharibiwa kabisa.
-
Ripoti: Miili mingi ya Wapalestina iliyokabidhiwa na Israel ina athari mateso na kunyofolewa viungo
Oct 18, 2025 01:02Wizara ya Afya ya Gaza imetangaza kuwa, miili mingi ya Wapalestina waliokabidhiwa na utawala wa Israel inaonyesha dalili za mateso makali, kunyongwa na kuporwa viungo vya mwili kama vile konea, figo na maini.