-
HRW: Serikali ya Biden inashirikiana na muungano vamizi katika kukiuka sheria za vita nchini Yemen
Apr 12, 2022 03:19Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema Rais wa Marekani atakuwa mshirika wa muungano vamizi katika kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Yemen iwapo ataendelea kuuza silaha kwa Imarati (UAE) na Saudi Arabia.
-
Jihad Islami: Siku zilizobaki za Ramadhani ni uwanja wa vita vikali na wavamizi
Apr 12, 2022 03:18Mjumbe wa ngazi ya juu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema kuwa, siku zilizosalia za mwezi mtukufu wa Ramadhani zitakuwa uwanja wa vita vikali na wavamizi wanaoikalia Quds kwa mabavu na kuongeza kuwa, ujinga wowote wa utawala ghasibu wa Israel utauangamiza utawala huo.
-
Nasrullah: Watu wa Palestina hawatashindwa katika mapambano yao dhidi ya Wazayuni
Apr 11, 2022 22:58Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, wananchi wa Palestina hawatashindwa katika mapambano yao ya ukombozi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
-
Hamas yasisitiza mapambano dhidi ya Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi
Apr 11, 2022 07:20Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameeleza kuwa moto wa mapambano dhidi ya Wazayuni unapaswa kukolezwa katika eneo lote la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Sana'a: UN ihitimishe ukiukaji mkubwa wa usitishaji vita wa muungano Saudia
Apr 11, 2022 03:47Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ametaka kuhitimishwa ukiukaji wa usitishaji vita huko Yemen unaofanywa na muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia.
-
"Mapambano ya Wapalestina yameingia katika marhala mpya"
Apr 10, 2022 22:05Mkuu wa Kituo cha Intifadha ya Palestina na Quds katika Baraza la Kuratibu Tablighi ya Kiislamu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Mapambano ya Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yameingia katika marhala mpya.
-
Bunge la Pakistani lapiga kura ya kutokuwa na imani na Imran Khan
Apr 10, 2022 22:05Baada ya wiki kadhaa za mivutano ya kisiasa nchini Pakistan, hatimaye wabunge wa mrengo wa upinzani bungeni wamepitisha mswada wa kutokuwa na imani na serikali ya Pakistani inayoongozwa na Waziri Mkuu Imran Khan.
-
Iraq: Kambi ya Marekani inayowahifadhi magaidi mashariki mwa Syria inapaswa kuvunjwa
Apr 10, 2022 06:38Afisa wa ngazi ya juu wa usalama wa Iraq ametoa wito wa kuvunjwa kambi ya wakimbizi inayodhibitiwa na wanamgambo wa Kikurdi wanaoungwa mkono na Marekani karibu na mpaka wa Iraq nchini Syria, akisema kambi hiyo inayohifadhi maelfu ya magaidi wa Daesh ni tishio halisi kwa nchi yake.
-
Utawala wa Kizayuni; sababu kuu ya machafuko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu
Apr 10, 2022 03:21Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameutaja utawala wa Kizayuni kuwa chanzo cha machafuko yote yanayoendelea katika ardhi za Wapalestina unazozikaliwa kwa mabavu.
-
Marekani yafanya mazoezi ya kijeshi Syria kinyume cha sheria
Apr 10, 2022 03:16Askari wa Jeshi la Marekani wamefanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na kundi la wanamgambo wanaojulikana kama Kurdish-Arab Syrian Democratic Forces (SDF) katika kisima cha mafuta cha Al-Omar katika eneo la Deir Ez-Zor katika ardhi ya Syria.