Hamas yasisitiza mapambano dhidi ya Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i82398-hamas_yasisitiza_mapambano_dhidi_ya_wazayuni_katika_ukingo_wa_magharibi
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameeleza kuwa moto wa mapambano dhidi ya Wazayuni unapaswa kukolezwa katika eneo lote la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 11, 2022 07:20 UTC
  • Fawzi Barhoum
    Fawzi Barhoum

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameeleza kuwa moto wa mapambano dhidi ya Wazayuni unapaswa kukolezwa katika eneo lote la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Ni baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuzidisha mashinikizo na jinai zake dhidi ya Wapalestina sambamba na kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, jambo ambalo limepelekea kuongezeka mapambano ya Wapalestina na operesheni za kujitolea kufa shahidi.

Fawzi Barhoum, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, amesema leo Jumatatu kwamba harakati hiyo inawategemea mashujaa wa Ukingo wa Magharibi kwa ajili ya kulisaidia eneo la Jenin.

Barhoum ameongeza kuwa: "Operesheni za wanamapambano wa Palestina zilizofanywa na mashujaa kama Zia Hamarsheh na Raad Hazem zinapaswa kuwatia moyo vijana katika Ukingo wa Magharibi."Palestina

Palestina

Msemaji wa Hamas amesema kuwa, operesheni za muqawama ni wajibu wa kidini na kitaifa na kwamba yeyote mwenye silaha anapaswa kufungua medani mpya katika mapambano dhidi ya adui Mzayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Amesisitiza kuwa hatua hiyo ni jibu halisi la Wapalestina kwa jinai zinazofanywa na Wazayuni maghasibu.

Jana asubuhi (Jumapili, Aprili 10), wanajeshi wa Israel walishambulia miji na vijiji kadhaa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, vikiwemo Jenin, Nablus, Tulkarm na Jeriko na kuwafyatulia risasi raia wa maeneo hayo. Wapalestika watatu akiwemo Ghada Ibrahim Sabatin, 47, mama wa watoto sita, wameuwa shahidi katika mashambulizi hayo ya wanajeshi wa Israel yaliyopamba moto sambamba na kuanza mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.