Marekani yafanya mazoezi ya kijeshi Syria kinyume cha sheria
Askari wa Jeshi la Marekani wamefanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na kundi la wanamgambo wanaojulikana kama Kurdish-Arab Syrian Democratic Forces (SDF) katika kisima cha mafuta cha Al-Omar katika eneo la Deir Ez-Zor katika ardhi ya Syria.
Wanajeshi wa Marekani na waitifaki wao wako kinyume cha sheria kaskazini na mashariki mwa Syria kwa muda mrefu ambapo wanahusika katika uporaji wa utajiri wa mafuta na nafaka sambamba na kutekeleza hujuma dhidi ya raia na wanajeshi wa Syria katika eneo hilo.
Mazoezi hayo ya kijeshi yamefanyika siku chache baada ya kituo cha jeshi la Marekani kushambuliwa katika kisima cha mafuta cha Al Omar.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Faisal al Mikdad alisema uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Syria ni kinyume cha sheria.
Mgogoro wa Syria ulianza mwaka 2011 wakati magaidi wa kimataifa, wakipata himaya ya Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wao waliposhambulia nchi hiyo ya Kiarabu kwa lengo la kuupa nguvu zaidi utawala wa Kizayuni wa Israe. Kwa muda mrefu Syria imekuwa kituo cha harakati za kupigania ukombozi wa Palestina.
Magaidi na wanamgambo wanaoendesha kampeni ya kuiangusha serikali ya Syria ni pamoja na kundi la ISIS au Daesh na wanamgambo wa SDF ambao wote wanapata himaya ya Marekani.
Katika hotuba yake ya kampeni za urais mwaka 2016, Hilary Clinton aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alikiri kuwa Washington ilianzisha makundi ya magaidi wakufurishaji kama vile Al Qaeda. Naye rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliwahi kutangaza kuwa rais aliyemtangulia Barack Obama ndiya aliyeanzisha kundi la kigaidi la ISIS.