-
Nasrullah: Iran ni nguvu kubwa kieneo na yenye taathira kubwa duniani
Feb 09, 2022 03:26Katibu Mkuu wa Chama cha Hizbullah cha nchini Lebanon ameashiria furaha kubwa waliyokuwanayo wananchi wa Iran wakati wa kurejea nchini Imam Khomeini (MA) kutoka uhamishoni na kusema hiyo ni moja ya nukta za kuvutia zaidi katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanayojulikana kama Alfajiri Kumi.
-
UN yataka kufanyika uchunguzi kuhusu wanaharakati wa kike waliotoweka Afghanistan
Feb 08, 2022 23:28Msemaji wa Umoja wa Mataifa amebainisha wasiwasi wa umoja huo kuhusu kukosekana taarifa kuhusiana na hali ya wanaharakti wa kike waliotoweka huko Afghanistan na kutaka kuitaka serikali ya Taliban kufanya uchunguzi katika uwanja huo.
-
Karibu Wayemen elfu nne ni wahanga wa mabomu ya vishada ya Saudia na washirika wake
Feb 08, 2022 08:48Mabomu ya vishada ya muungano vamizi katika vita vya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia yanayovurumishwa kwa wananchi wasio na hatia hadi kufikia mwaka jana wa 2021 yameuwa raia karibu elfu nne wa nchi hiyo.
-
Syria yaipongeza AU kwa kusimamisha uanachama wa Israel katika jumuiya hiyo
Feb 07, 2022 23:19Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Syria imekaribisha uamuzi wa Umoja wa Afrika wa kusimamisha hadhi ya uanachama mwangalizi ya utawala wa Kizayuni Israel katika jumuiya hiyo.
-
Kuwait yapiga marufuku filamu ya 'Death on the Nile' iliyoigizwa na Muisraeli
Feb 07, 2022 23:19Kuwait imepiga marufuku kuonyeshwa kwa filamu ya Kimarekani ya Death on the Nile, iliyotengenezwa kutoka kwenye riwaya yenye majina ya Agatha Christie na kuchezwa na mwigizaji wa Israel, Gal Gadot.
-
Bunge la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu launga mkono kufukuzwa Israel katika Umoja wa Afrika
Feb 07, 2022 09:21Bunge la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) limeunga mkono na kusifu hatua ya Umoja wa Afrika ya kukataa utawala wa Kizayuni wa Israel kupatiwa hadhi ya mwanachama mwangalizi katika umoja huo.
-
Al Houthi: Uamuzi wa AU dhidi ya Israel ni pigo kubwa kwa wanaopatana na Wazayuni
Feb 07, 2022 03:52Mjumbe mmoja mwandamizi wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa, hatua ya Umoja wa Afrika (AU) ya kuutimua utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye umoja huo ni pigo kubwa kwa wale wanaojipendekeza kwa utawala huo dhalimu.
-
Viongozi wa Qatar na Imarati waonana kwa mara ya kwanza tangu Saudia ilipoanzisha mgogoro dhidi ya Doha
Feb 07, 2022 03:48Amir wa Qatar, ameonana na mrithi wa kiti cha ufalme wa Umoja wa Falme za Kiarabu pembeni mwa sherehe za ufunguzi wa mashindano ya msimu wa baridi kali ya mjini Beijing, China ikiwa ni mara ya kwanza tangu nchi nne za Kiarabu zikiongozwa na Saudi Arabia, zilipokata uhusiano wao wote na Qatar.
-
Wapalestina waishukuru AU kwa kuifukuza Israel kwenye umoja huo wa Afrika
Feb 07, 2022 01:01Harakati za muqawama wa Palestina za Hamas na Jihad al Islami zimeushukuru Umoja wa Afrika (AU) kwa kuutimua utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye umoja huo na kusema kuwa, hatua hiyo ni pigo kwa zile nchi zinazotangaza uhusiano wa kawaida na utawala huo katili.
-
Kongresi ya Taifa ya Yemen: Uhusiano na Ansarullah ni muhimu na wa kimkakati
Feb 06, 2022 23:26Kongresi ya Taifa ya Yemen imesema kuwa upo uhusiano imara kati ya viongozi wa chama hicho na harakati ya Ansarullah na kwamba propaganda na hujuma za vyombo vya habari za mamluki adui na wanaofanya khiyana haziathiri kivyovyote uhusinao wao huo.