UN yataka kufanyika uchunguzi kuhusu wanaharakati wa kike waliotoweka Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i80136-un_yataka_kufanyika_uchunguzi_kuhusu_wanaharakati_wa_kike_waliotoweka_afghanistan
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amebainisha wasiwasi wa umoja huo kuhusu kukosekana taarifa kuhusiana na hali ya wanaharakti wa kike waliotoweka huko Afghanistan na kutaka kuitaka serikali ya Taliban kufanya uchunguzi katika uwanja huo.
(last modified 2026-02-03T09:36:48+00:00 )
Feb 09, 2022 02:58 UTC
  • UN yataka kufanyika uchunguzi kuhusu wanaharakati wa kike waliotoweka Afghanistan

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amebainisha wasiwasi wa umoja huo kuhusu kukosekana taarifa kuhusiana na hali ya wanaharakti wa kike waliotoweka huko Afghanistan na kutaka kuitaka serikali ya Taliban kufanya uchunguzi katika uwanja huo.

Katika miezi ya karibuni wanawake nchini Afghanistani walifanya maandamano mara kadhaa katika baadhi ya miji ya nchi hiyo ikiwemo katika mji mkuu Kabul wakilalamikia hatua ya serikali ya Taliban ya kuwawekea vizuizi na hivyo kushindwakupata elimu na kufanya kazi. Wanawake hao waliitaka serikali ya Taliban iheshimu  haki yao yao hiyo ya kimsingi. Hata hivyo kundi hilo hadi sasa halijachukua hatua zozote za kuwaridhisha wanawake nchini Afghanistan licha ya wao kulalamika na jamii ya kimataifa kuitaka Taliban kuondoa vizuizi hivyo tajwa dhidi ya wanawake.  

Stephen Dujaric Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja jwa Mataifa jana Jumanne alieleza kuwa: Ofisi ya Haki za Binadamu ya umoja huo imetangaza kuwa tangu  kutoweka wiki tatu zilizopita wanaharakati wa kike wanne na familia zao, hadi sasa hakuna taarifa zozote kuhusu mahali walipo raia hao wa Afghanistan. 

Stephen Dujaric, Msemaji wa Katibu Mku wa UN 

Ameongeza kuwa, raia hao walitekwanyara au kutiwa nguvuni na kupelekwa mahali kusikojulikana wakihusishwa na maandamano ya karibuni ya kupinga ukiukaji wa haki za wanawake hukko Afghanistan.   

Msemaji wa Umoja wa Katibu Mkuu wa Mataifa amebainisha kuwa umoja huo unawataka viongozi wa Afghanistan kuwasilisha taarifa zinazohitajika na za lazima kuhusu suala hilo la kutoweka wanaharakati hao wa kike sambamba na kufanya uchunguzi wa kina na wa wazi kuhusu hatima ya raia hao.