-
Wimbi jipya la corona latua pia nchini Saudi Arabia, mamia ya watu waambukizwa
Jun 30, 2021 01:48Wizara ya Afya ya Saudi Arabia jana ilitangaza kuwa, watu 1,567 wamethibitishwa kukumbwa na ugonjwa wa COVID-19 katika kipindi cha siku moja nchini humo. Hilo lilikuwa ni tangazo rasmi kuwa Saudia imo kwenye wimbi jipya la maambukizi ya kirusi cha corona.
-
Kituo cha MOSSAD chashambuliwa Erbil huku Waziri wa Israel akiitembelea UAE
Jun 29, 2021 21:56Huku Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel akifanya safari ya kwanza ya kuutembelea Umoja wa Falme za Kiarabu, kambi ya Shirika la Kijasusi la Utawala huo wa Kizayuni (MOSSAD) imeshambuliwa kwa maroketi katika eneo la Erbil, kaskazini mwa Iraq.
-
Haniya na Nasrullah wajadili njia za kupata 'ushindi wa mwisho' dhidi ya Israel
Jun 29, 2021 21:53Viongozi wakuu wa mrengo wa muqawama wa Palestina na Lebanon wamejadili kipigo cha hivi karibuni cha Wapalestina wa Ukanda wa Gaza dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, sanjari na kubadilishana mawazo juu ya njia zinazopaswa kufuatwa ili kupata 'ushindi mutlaki' dhidi ya utawala huo haramu.
-
Misri: Kuhitimishwa uingiliaji wa nchi ajinabi; sharti la kurejeshwa amani Syria
Jun 29, 2021 06:38Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema katika kikao cha mawaziri wa muungano wa kimataifa unaodai kupambana na Daesh kwamba, sharti la kurejesha amani huko Syria ni kukomesha uingiliaji wa nchi ajinabi nchini humo.
-
Ilhan Omar alaumu shambulio ya Marekani dhidi ya makundi ya muqawama ya Iraq
Jun 28, 2021 22:12Mbunge Muislamu nchini Marekani ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya shambulizi katika mpaka wa Syria na Iraq na kusema kuwa, shambulio hilo ni siasa zilizofeli.
-
Makundi ya muqawama ya Iraq: Tutalipiza kisasi dhidi ya Marekani
Jun 28, 2021 06:13Makundi ya muqawama ya Iraq yametangaza kuwa, yatalipiza kisasi mashambulizi ya Marekani dhidi ya ngome za kundi la Hashdu Shaabi.
-
Habari za karibuni kuhusu shambulio la Marekani dhidi ya makundi ya mapambano ya Iraq
Jun 28, 2021 03:37Afisa mmoja wa Marekani amesema nchi hiyo ametumia ndege za kivita aina ya F15 na F16 kushambulia makundi ya mapambano ya Kiislamu katika maeneo ya mpaka wa Iraq na Syria.
-
Syria yaalani misimamo ya Marekani na utawala wa Kizayuni kuhusu Miinuko ya Golan
Jun 27, 2021 21:59Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria kwa mara nyingine tena imesisitiza kuwa eneo la Golan ni sehemu ya ardhi ya nchi hiyo na kueleza kuwa, mamlaka ya nchi hiyo kwa eneo la Golan haibadiliki kwa kupita muda na misimamo ya Marekani na utawala wa Israel haina taathira yoyote ya kisheria.
-
Ushirikiano wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Israel katika kuwakandamiza Wapalestrina
Jun 27, 2021 04:44Kuuawa shahidi mwanaharakati wa Kipalestina Nizar Banat mwenye umri wa miaka 42 na askari wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kumeongeza mashinikizo dhidi ya mamlaka hiyo na mkuu wake Mahmoud Abbas, ambapo sasa Wapalestina wanataka malaka hiyo ivunjwe na Rais Mahmoud Abbas ajiuzulu.
-
Palestina yataka kuwekwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Israel
Jun 26, 2021 22:07Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Palestina imelaani uhalifu unaoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Palestina na kutoa wito wa kuwekwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya utawala huo.