-
Wayemen waandamana kuinga mkono Ansarullah, wailaani UN
Jun 26, 2021 08:10Wananchi wa Yemen wamefanya maandamano kaskazini magharibi mwa nchi kulaani hatua ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kuiweka harakati ya muqawama ya Ansarullah katika orodha nyeusi ya eti taasisi zinazokiuka haki za watoto.
-
Nasrullah: Kuteka tovuti za muqawama kumefichua unafiki wa Marekani
Jun 26, 2021 08:05Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kitendo cha Marekani cha kuteka na kufunga tovuti kadhaa za vyombo vya habari vya kambi ya muqawama kimedhihirisha unafiki wa Marekani inayodai kuwa mtetezi mkubwa wa demokrasia na uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari.
-
Amnesty International yakiri polisi wa Israel wanafanya jinai dhidi ya Wapalestina
Jun 26, 2021 02:48Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limewashutumu polisi wa utawala wa Kizayuni kwa kufanya jinai nyingi dhidi ya Wapalestina.
-
Ansarullah: Hatujawahi na kamwe hatutafuti utambulisho wetu kutoka kwa Marekani
Jun 26, 2021 02:46Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen ametuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kusisitiza kuwa, harakati hiyo ya wananchi wa Yemen kamwe haijawahi kufikiria kutafuta utambulisho wake kutoka kwa Marekani na haina haja ya kutambuliwa rasmi na dola hilo la kiistikbari.
-
Upatanishi wa Hizbullah kwa ajili ya kupunguza mivutano ya kisiasa nchini Lebanon
Jun 25, 2021 22:00Vyanzo vya habari vimetangaza habari ya juhudi zinazofanywa na Chama cha Hizbullah ya Lebanon kwa madhumuni ya kuwapatanisha Rais na Spika wa Bunge la Lebanon na vile vile makundi ya kisiasa ya nchi hiyo kwa ajili ya kupunguza mivutano na kufikia muwafaka kuhusu namna ya kubuni serikali mpya ya nchi hyo.
-
Free Beacon: Marekani inatengua uamuzi wake wa kuitambua rasmi Miinuko ya Golan kuwa ni ardhi ya Israel
Jun 25, 2021 07:21Tovuti moja ya Marekani imeripoti kuwa, serikali ya Joe Biden imo katika mikakati ya kutengua uamuzi uliochukuliwa na serikali ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Donald Trump ya kutambua rasmi ardhi ya Miinuko ya Golan ya Syria kuwa ni sehemu ya ardhi inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni (Israel).
-
Hizbullah yalaani hatua ya Marekani kufunga tovuti za mrengo wa muqawama
Jun 25, 2021 03:19Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali hatua ya serikali ya Marekani kuteka na kufunga tovuti kadhaa za vyombo vya habari vya Iran na kieneo na kusema kitendo hicho ni jinai inayothibitisha sera za ukandamizaji zinazofuatwa na Washington.
-
Emir wa Qatar azungumza kwa simu na rais mteule wa Iran
Jun 25, 2021 03:14Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amefanya mazungumzo ya simu na rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Seyyed Ebrahim Raeisi.
-
Wananchi wa Jordan walalamikia kushikiliwa raia wa nchi hiyo katika jela za Saudi Arabia
Jun 24, 2021 08:23Familia za raia wa Jordan wanaoshikiliwa katika jela za kutisha za Saudi Arabia bila ya kufikishwa mahakamani , wamelalamikia vikali uamuzi wa Riyadh wa kuakihirisha kusikilizwa kesi za Wajordan hao. Familia hizo zimelaani hatua ya Saudia ya kurefusha muda wa kukaa korokoroni raia hao wa Jordan huko Saudia bila ya sababu yoyote.
-
Kilio cha watoto wa Yemen kufuatia Umoja wa Mataifa kuzikingia kifua nchi vamizi
Jun 24, 2021 05:02Juzi Jumanne watoto wa Yemen waliandamana kulalamikia kuendelea jinai zisizo za kibinadamu za utawala wa Saudi Arabia dhidi ya wananchi wa Yemen wasio na hatia na kukaa kimya Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa bila kuchukua hatua mkabala wa jinai hizo.