Wayemen waandamana kuinga mkono Ansarullah, wailaani UN
Wananchi wa Yemen wamefanya maandamano kaskazini magharibi mwa nchi kulaani hatua ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kuiweka harakati ya muqawama ya Ansarullah katika orodha nyeusi ya eti taasisi zinazokiuka haki za watoto.
Wananchi wa Yemen sambamba na kutangaza uungaji mkono wao kwa harakati hiyo ya mapambano, wamekitaja kitendo hicho cha Guterres cha kuiweka Ansarullah katika orodha yake nyeusi ya kila mwaka kuwa ni cha kipumbavu.
Katika maandamano hayo yaliyofanyika katika mji wa Sa’ada wa kaskazini magharibi mwa nchi, maelfu ya Wayemen wamemkosoa vikali Katibu Mkuu wa UN ya kuiweka Ansarullah katika orodha hiyo nyeusi, huku akiliondoa jina la Saudi Arabia katika jalada hilo.
Waandamanaji hao aghalabu yao wakiwa watoto watoto wamesema ni kinaya kwa Guterres kuiiondoa Riyadh katika orodha hiyo, licha ya kuwa utawala wa Aal-Saud unaongoza muungano vamizi wa kijeshi unaoaua maelfu ya watoto wa Kiyemen kila uchao.
Wananchi wa Yemen walioshiriki kwenye maandamano hayo wamesema kwenye taarifa ya pamoja kuwa: Tunataja hatua ya UN ya kuwatuhumu Wayemen wanauana wenye kwa wenywe huku akiiondolewa Saudi Arabia lawama, kuwa ya kipumbavu. Taarifa zinazotolewa na taasisi hiyo haina umuhimu wowote kwetu tena.
Waandamanaji hao wamesema wanautazama Umoja wa Mataifa kama mshirika wa muungano vamizi wa Saudia katika jinai zake dhidi ya wananchi wa Yemen, huku wakilaani kitendo cha UN cha kujaribu kuupa uhalali muungano huo.