Ansarullah: Hatujawahi na kamwe hatutafuti utambulisho wetu kutoka kwa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i71684-ansarullah_hatujawahi_na_kamwe_hatutafuti_utambulisho_wetu_kutoka_kwa_marekani
Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen ametuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kusisitiza kuwa, harakati hiyo ya wananchi wa Yemen kamwe haijawahi kufikiria kutafuta utambulisho wake kutoka kwa Marekani na haina haja ya kutambuliwa rasmi na dola hilo la kiistikbari.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 26, 2021 02:46 UTC
  • Ansarullah: Hatujawahi na kamwe hatutafuti utambulisho wetu kutoka kwa Marekani

Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen ametuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kusisitiza kuwa, harakati hiyo ya wananchi wa Yemen kamwe haijawahi kufikiria kutafuta utambulisho wake kutoka kwa Marekani na haina haja ya kutambuliwa rasmi na dola hilo la kiistikbari.

Muhammad al Bukhaiti ameandika kwenyeb ukurasa wake wa Twitter kuwa: "Sisi kamwe hatujawahi kutafuta utambulisho wetu kutoka kwa Martekani bali tunachopigania sisi ni kurejesha utawala na uhuru wa Yemen na kukomboa kila shibri ya ardhi ya nchi yetu."

Vile vile amesema, harakati ya kujitolea ya wananchi wa Yemen yaani Ansarullah imetoa muhanga vitu vyake vingi vya thamani katika njia ya Allah na imepoteza roho za watu wake wengi katika mapambano ya kihistoria na yasiyo na kjfani ya kuihami Yemen na watu wake.

Amesema, tunachokitaka sasa hivi kutoka kwa nchi vamizi zinazoongozwa na Marekani, ni kukomeshwa uvamizi wao, kuacha kuizingira Yemen, kutoka askari wa kigeni na kuheshimiwa matakwa na maamuzi ya wananchi wa Yemen.

Tim Linder King

 

Alkhamisi usiku, Tim Linder King, mjumbe maalumu wa Marekani katika masuala ya Yemen alitangaza kuwa, Washington inaitambua harakati ya kujitolea ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah kuwa ni harakati ya kisheria inayopasa kushirikishwa katika utatuzi wa mgogoro wa nchi hiyo.

Kwa upande wake, Muhammad Ali al Houthi, Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen naye amejibu matamshi hayo ya mjumbe maalumu wa Marekani kuhusu Yemen kwa kusema: "Utambulisho wa Yemen unatokana na nguvu na muqawama wa wananchi wake."