Amnesty International yakiri polisi wa Israel wanafanya jinai dhidi ya Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i71688-amnesty_international_yakiri_polisi_wa_israel_wanafanya_jinai_dhidi_ya_wapalestina
Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limewashutumu polisi wa utawala wa Kizayuni kwa kufanya jinai nyingi dhidi ya Wapalestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 26, 2021 02:48 UTC
  • Amnesty International yakiri polisi wa Israel wanafanya jinai dhidi ya Wapalestina

Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limewashutumu polisi wa utawala wa Kizayuni kwa kufanya jinai nyingi dhidi ya Wapalestina.

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Tasnim ambalo limeongeza kuwa, usiku wa kuamkia jana, shirika la Amnesty International liliushutumu utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai kubwa unazowafanyia Wapalestina na kuongeza kuwa, polisi wa Israel wanafanya ukandamizaji mkubwa, ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa kizazi, kuwatia mbaroni kwa umati Wapalestina na kutumia vibaya nguvu dhidi ya watu wa kawaida, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza jinai chungu nzima dhidi ya Wapalestina wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, utawala wa Kizayuni hauwalindi wala kuwasaidia Wapalestina hata wenye uraia wa Israel wakati wanaposhambliwa na walowezi Wazayuni.

Rais Mpalestina chini ya ukandamizaji wa mabuti ya kijeshi ya wanajeshi makatili wa Israel

 

Shirika la Amnesty International pia limeandika, tangu tarehe 13 Mei 2021 hadi hivi sasa, walowezi wa Kizayuni wameshaharibu magari 90 ya Wapalestina na mara chungu nzima wanawalenga kwa mawe Wapalestina hata wakiwa ndani ya nyumba zao.

Saleh Hijazi, Naibu Mkuu wa Ofisi Amnesty International ya eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini amesema kuwa, ushahidi uliokusanywa na shirika hilo unaonesha kuwa, Wazayuni wanaendelea kufanya mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya Wapalestina na vile vile kunyamazisha sauti ya kila mtu anayesimama kupinga na kulaani ubaguzi, dhulma na ukandamizaji unaofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina.