-
Wasiwasi waongezeka, Wazayuni wakijiandaa kufanya maandamano 14 ya kichochezi leo Jumatatu
Jun 21, 2021 02:21Baada ya walowezi wa Kizayuni kutangaza nia yao ya kufanya maandamano 14 ya kichochezi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan leo Jumatatu, kamati za muqawama za wananchi wa Palestina nazo zimetoa mwito kwa Wapalestina kujitokeza katika medani ya kupambana na chokochoko za Wazayuni hao.
-
Hamas: Msikiti wa al-Aqsa utakombolewa karibuni hivi
Jun 20, 2021 22:24Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema taifa la Palestina karibuni hivi litaukomboa Msikiti mtukufu wa al-Aqsa, huko Baitul Muqaddas inayokaliwa kwa mabavu.
-
Ansarullah yakosoa kauli ghalati ya jenerali wa kijeshi wa US dhidi ya Yemen
Jun 20, 2021 22:19Mwanachama wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amemkosoa vikali Kamanda Mkuu wa Kamandi Kuu ya Kijeshi ya Marekani (CENTCOM) kwa kutoa matamshi yasiyo na msingi kuwa Sanaa imekataa kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kusisitiza kuwa, afisa huyo wa Washington hana ufahamu wowote kuhusu siasa.
-
Wazayuni wauhujumu tena Msikiti wa Al Aqsa
Jun 20, 2021 07:55Waloweiz wa Kizayuni wameuhujumu kwa mara nyingine Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) huku wakipata himaya ya askari wa utawala haramu wa Israel wakati wakitekeleza jinai hiyo.
-
Jeshi la Yemen latungua ndege isiyo na rubani ya Marekani
Jun 20, 2021 07:40Jeshi la Yemen limetangaza kuwa limefanikiwa kutungua ndege ya kijasusi ya Jeshi la Marekani katika anga ya mkoa wa Ma'rib.
-
Makundi ya muqawama ya Palestina yautahadharisha utawala wa Kizayuni
Jun 20, 2021 03:45Makundi ya muqawama ya Palestina yametangaza kuwa hayautauruhusu utawala ghasibu wa Kizayuni uutwishe muqawama masharti yake au kuufanya Ukanda wa Ghaza uwe katika hali ya kutengwa.
-
Ansarullah: Tuhuma za Guterres kuhusu ukiukaji wa haki za watoto ni fedheha na aibu
Jun 20, 2021 03:42Idara ya Siasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen imetangaza kuwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesajili jina lake na taasisi hiyo katika orodha ya fedheha na aibu kwa kuliweka jila la harakati hiyo katika orodha ya makundi yanayokiuka haki za watoto duniani.
-
Wapalestina 160 wanateseka katika jela za Saudi Arabia hivi sasa
Jun 19, 2021 21:53Shirika la habari la "Palestine Today" limetangaza kuwa, sasa hivi kuna Wapalestina 160 wanaoteseka katika jela za ukoo wa Aal Saud nchini Saudi Arabia. Wapalestina hao wanashikiliwa kwenye jela hizo za Saudi Arabia kwa tuhuma za kuwa wanachama wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.
-
Saudia yapanga kuwanyonga vijana 40 wa Kishia
Jun 19, 2021 08:07Wanaharakati wa haki za binadamu wameonya kuwa, utawala wa Aal-Saud unapanga kuwanyonga makumi ya vijana Waislamu wa madhehebu ya Shia mkoani Qatif mashariki mwa Saudi Arabia.
-
Mlingano wa Quds na makundi ya muqawama Magharibi mwa Asia
Jun 18, 2021 21:55Harakati ya Kata'ib Hizbullah (Brigedi za Hizbullah) ya Iraq imetoa taarifa na kuashiria kuendelea jinai na chokochoko za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina na mji wa Quds (Jerusalem) na kutangaza rasmi kuingia katika kadhia ya 'Mlingano wa Quds' kwa lengo la kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel.