-
Oxfam: Silaha za Uingereza zinazouzwa Saudia zinarefusha vita nchini Yemen
Feb 22, 2021 23:19Shirika la misaada ya kibinadamu la Oxfam limetangaza kuwa, uuzaji wa silaha za Uingereza kwa utawala wa Saudi Arabia unarefusha vita vya muungano unaoongozwa na serikali ya Riyadh dhidi ya taifa la Yemen.
-
Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu: Sehemu kubwa ya Madaesh wa kujiripua wameingia Iraq kutokea Syria
Feb 22, 2021 23:14Mkuu wa Umoja wa Maulamaa wa Kiislamu katika mkoa wa Diyala nchini Iraq amesema kuwa, sehemu kubwa ya magaidi wa Daesh (ISIS) wa kujiripua kwa mabomu wameingia nchini Iraq wakitokea Syria.
-
Vipengele vya "Hati ya Heshima ya Palestina" kwa ajili ya kukabiliana na mapatano ya kuanzisha uhusiano rasmi na Israel
Feb 22, 2021 09:07Makundi ya Kipalestina, jana Jumapili Februari 21 yalikutana Ukanda wa Gaza na kusaini "Hati ya Heshima ya Palestina" katika kuonyesha upinzani wao dhidi ya uanzishaji uhusiano wa kawaida wa vyombo vya habari na utawala haramu wa Kizayuni.
-
Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi lataka hitilafu za Somalia zitatuliwe kwa njia za amani
Feb 22, 2021 04:33Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi limezungumzia matukio ya vitendo vya utumiaji mabavu na mauaji ya hivi karibuni katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kutoa wito wa kupatiwa ufumbuzi hitilafu zinazoikabili nchi hiyo kwa njia za amani.
-
Vikosi vya Yemen vimeidhibiti jela yenye mfungamano na Mansour Hadi huko Ma'rib
Feb 21, 2021 23:25Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen imetengakuwa, jeshi la Yemen na harakati ya Ansarullah vimeidhibiti jela ya wanamgambo wenye mfungamano na Mansour Hadi Rais wa Yemen aliyejiuzulu. Jela hiyo imedhibitiwa huko katika mji wa Ma'rib.
-
Shughuli za siri za nyuklia za Wazayuni katika kivuli cha kimya na undumakuwili wa Magharibi
Feb 21, 2021 22:59Tarehe 8 Mei 2019, mwaka mmoja baada Marekani kujitoa bila ya sababu katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na baada ya kuthibiti kutokuwa na faida njia zilizopendekezwa na Ulaya za kudhamini maslahi ya Iran ndani ya mapatano hayo, Jamhuri ya Kiislamu iliamua kupunguza kwa awamu 5, sehemu ya ahadi zake ndani ya JCPOA kama vinavyosema vifungu vya 26 na 36 vya makubaliano hayo ya kimataifa.
-
Serikali ya Mansour Hadi: Wananchi wamejiunga na Ansarullah Yemen
Feb 21, 2021 00:45Waziri wa Habari, utamaduni na utalii wa serikali iliyojiuzulu ya Yemen amekiri kwamba wananchi wa mkoa wa Ma'rib wamejiunga na jeshi na kamati za kujitolea za wananchi na kuwataka wakazi wa mkoa huo wasiache vijana wao kujiunga na kamati hizo za kujitolea ambazo ni maarufu kwa jina la Ansarullah.
-
Saudia yazidi kushutumiwa kwa kuvunja haki za binadamu
Feb 21, 2021 00:43Dada wa mwanaharakati mmoja wa masuala ya kijamii wa Saudi Arabia ameushutumu vikali utawala wa ukoo wa Aal Saud kwa kuwatesa na kuwakandamiza wakosoaji wa utawala huo wa kiimla.
-
Mfadhili mkuu wa kifedha wa Daesh atiwa mbaroni mkoani Diyala, Iraq
Feb 20, 2021 04:35Idara ya Intelijinsia ya Jeshi la Iraq imetangaza habari ya kutiwa mbaroni mfadhili mkuu wa kifedha wa kundi la Daesh mkoani Diyala mashariki mwa nchi hiyo.
-
Kiongozi wa Ansarullah: Yemen haitawekwa chini ya mamlaka ya Saudia, Marekani wala Israel
Feb 20, 2021 00:22Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa watu wa nchi hiyo hawatawekwa chini ya mamlaka ya Saudi Arabia, Imarati, Marekani au utawala wa Kizayuni wa Israel.