-
Israel inapanua kwa siri kituo chake cha silaha za nyuklia
Feb 19, 2021 23:28Picha mpya za satalaiti zinaonyesha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao ni mmiliki pekee wa silaha za nyuklia Asia Magharibi, unatekeleza mradi wa kupanua kituo chake cha siri cha nyuklia katika Jangwa la Negev.
-
Vita ya Maʼrib, muungano wa Saudi Arabia na Daesh na jitihada za kukimbia kinamasi cha Yemen
Feb 19, 2021 23:25Sambamba na kuendelea kusonga mbele wapiganaji wa makundi ya kujitolea ya Yemen kuelekea Maʼrib, Saudi Arabia imeamua kutuma askari wa ziada nchini Yemen na kutumia wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh huku nchi za Kiarabi zikifanya juhudi kubwa za kidiplomasia za kuzuia fedheha na kushindwa Riyadh na waitifaki wake katika kinamasi cha Yemen.
-
Wabunge wa Iraq wataka uingiliaji wa Marekani katika masuala ya nchi hiyo ukomeshwe
Feb 19, 2021 10:33Wabunge kadhaa wa Iraq wametoa indhari kuhusu uingiliaji wa Marekani hasa katika kadhia ya uchaguzi ujao wa bunge na katika masuala ya kijeshi na kiusalama ya nchi hiyo.
-
Wanaharakati wa haki za binadamu watiwa wasiwasi na ukiukaji mkubwa wa haki za watoto nchini Bahrain
Feb 19, 2021 10:19Wanaharakati wa haki za binadamu na waangalizi wa kimataifa wamesema wanatiwa wasiwasi na hatua za utawala wa Aal Khalifa za kuwakamata na kuwaweka korokoroni watoto wadogo nchini Bahrain.
-
Hamas: Kubadilishana mateka, njia pekee ya Israel kuwapata mateka wake
Feb 19, 2021 03:41Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni itawapata wanajeshi wake waliotekwa nyara kupitia tu mpango wa kubadilishana mateka.
-
UN: Watoto wa Kiyemen laki nne chini ya miaka mitano wana utapiamlo
Feb 19, 2021 00:50Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu jana aliitaja hali ya kibinadamu huko Yemen kuwa ya maafa na kutangaza kuwa, hivi asa kuna karibu watoto laki nne chini ya miaka mitano wenye utapiamlo nchini humo.
-
Video ya Hizbullah iliyokashifu vituo vya kijeshi vya Israel ndani ya miji yazusha taharuki
Feb 18, 2021 22:54Kwa mara ya kwanza, harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa mkanda wa video unaoonyesha kambi na vituo vya kijeshi vya jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndani ya miji ya ardhi hizo za Palestina unazozikalia kwa mabavu.
-
DAESH (ISIS) yakiri kuwa inapigana bega kwa bega na Saudia katika vita dhidi ya Yemen
Feb 18, 2021 22:53Kundi la kigaidi la DAESH (ISIS) limetangaza kuwa linashiriki katika operesheni ya kijeshi na vita dhidi ya harakati ya Ansarullah ya Yemen katika eneo la Ma'rib.
-
Kuendelea mapigano kati ya Imarati na Saudia huko Yemen
Feb 18, 2021 06:04Mamluki wenye mfungamano na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko kusini mwa Yemen wamevishambulia vikosi vya serikali iliyojiuzulu ya Yemen ya Abdrabbuh Mansur Hadi inayoungwa mkono na Saudi Arabia wakati vilipokuwa vikielekea katika mkoa wa Maarib mashariki mwa Yemen.
-
Silaha za NATO zakamatwa katika makao ya Daesh Homs, nchini Syria
Feb 18, 2021 04:46Jeshi la Syria limegundua ghala la silaha ziliundwa na Shirila la Kujihami la Nchi za Magharibi (NATO) katika mji wa Homs baada ya kuua magaidi kadhaa wa kundi la Daesh katika eneo hilo.