Kuendelea mapigano kati ya Imarati na Saudia huko Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i66994-kuendelea_mapigano_kati_ya_imarati_na_saudia_huko_yemen
Mamluki wenye mfungamano na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko kusini mwa Yemen wamevishambulia vikosi vya serikali iliyojiuzulu ya Yemen ya Abdrabbuh Mansur Hadi inayoungwa mkono na Saudi Arabia wakati vilipokuwa vikielekea katika mkoa wa Maarib mashariki mwa Yemen.
(last modified 2026-02-25T07:04:48+00:00 )
Feb 18, 2021 09:34 UTC
  • Kuendelea mapigano kati ya Imarati na Saudia huko Yemen

Mamluki wenye mfungamano na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko kusini mwa Yemen wamevishambulia vikosi vya serikali iliyojiuzulu ya Yemen ya Abdrabbuh Mansur Hadi inayoungwa mkono na Saudi Arabia wakati vilipokuwa vikielekea katika mkoa wa Maarib mashariki mwa Yemen.

Baadhi ya duru za habari za kuaminika leo zimeripoti kuwa, mamluki wenye silaha wenye mfungamano na kundi la Baraza la Mpito la Kusini wameushambulia msafara wa magari ya kijeshi ya vikosi vya serikali iliyojiuzulu ya Mansur Hadi inayoungwa mkono na Saudi Arabia katika mkoa wa Abyan ambavyo viilikuwa vikielekea mkoani Maarib. 

Abdu Rabbuh Mansour Hadi 

Duru hizo za habari zimeeleza kuwa, vikosi vya Mansur Hadi vilikuwa na lengo la kufika mkoani Maarib ambako mapigano yalikuwa yakijiri kati ya vikosi hivyo na vile vya jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen.  

Wapiganaji watatu wa Mansur Hadi wamejeruhiwa katika mapigano hayo na waliosalia wamesonga mbele kuelekea Maarib. Kusonga mbele huko kkwa jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi katika siku za karibuni katika mji wa kistratejia wa Maarib huko mashariki mwa Yemen kumeitia hofu serikali iliyojiuzulu na muungano vamizi wa Saudia unaoungwa mkono na Marekani.