Silaha za NATO zakamatwa katika makao ya Daesh Homs, nchini Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i66990-silaha_za_nato_zakamatwa_katika_makao_ya_daesh_homs_nchini_syria
Jeshi la Syria limegundua ghala la silaha ziliundwa na Shirila la Kujihami la Nchi za Magharibi (NATO) katika mji wa Homs baada ya kuua magaidi kadhaa wa kundi la Daesh katika eneo hilo.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Feb 18, 2021 08:16 UTC
  • Silaha za NATO zakamatwa katika makao ya Daesh Homs, nchini Syria

Jeshi la Syria limegundua ghala la silaha ziliundwa na Shirila la Kujihami la Nchi za Magharibi (NATO) katika mji wa Homs baada ya kuua magaidi kadhaa wa kundi la Daesh katika eneo hilo.

Televisheni ya Russia Today imemnukuu kamanda wa jeshi la Russia akisema kuwa, jeshi la Syria limefanikiwa kuwaua magaidi wanne wa kundi la Daesh na kunasa ghala kubwa la silaha kufuatia operesheni iliyofanywa na jeshi hilo katika mji wa Homs likisaidiwa na ndege zisizo na rubani za Russia. 

Ripoti zinasema kuwa magaidi hao walikuwa na kazi ya kulinda ghala hilo la silaha za Daesh zilizoundwa na shirika la NATO.

Katika operesheni hiyo jeshi la Syria pia limenasa silaha zilizotengenezwa katika nchi za Magharibi na karibu kilo 40 za mada za milipuko, madawa na vyakula.

Nchi zaMagharibi zinashirikiana na magaidi wa kundi la Daesh

Kamanda huyo wa jeshi la Russia ameongeza kuwa, harakati za kundi la Daesh zimeongezeka sana katika eneo hilo linalokaribiana na al Tanf tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Eneo hilo la Tanf nchini Syria linakaliwa kwa mabavu na majeshi vamizi ya Marekani na makundi ya kigaidi yanayopigana vita dhidi ya serikali halali ya Syria.

Wataalamu wanasema jeshi la Marekani linatoa mafunzo ya kijeshi kwa wanachama wa makundi ya kigaidi husuan Daesh katika eneo hilo la al Tanf na baadaye kuwatuma katika maeneo mbalimbali ya Syria na Iraq.