-
Safari ya Waziri Mkuu wa Pakistan nchini Afghanistan; fursa ya kuimarisha uhusiano wa nchi mbili
Nov 19, 2020 04:28Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan leo amefanya ziara ya siku moja ya kuitembelea Afghanistan kufuatia mwaliko rasmi aliopewa na Rais Ashraf Ghani wa nchi hiyo. Imeelezwa kwamba katika ziara yake hiyo ya siku moja, Waziri Mkuu wa Pakistan atafanya mazungumzo na kubadilishana mawazo na viongozi wa Kabul kuhusu amani ya nchi hiyo na namna ya kustawisha ushirikiano wa kisiasa, kiusalama na kiuchumi kati ya nchi mbili.
-
Maseneta wa Marekani wapanga kuzuia mauzo ya silaha kwa Imarati
Nov 19, 2020 03:45Maseneta watatu wa Marekani wamesema wanataka kuwasilisha miswada ya kuizuia serikali ya hivi sasa ya Donald Trump kuiuzia silaha Imarati.
-
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa: Israel ni dola vamizi
Nov 19, 2020 02:50Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio linaloutaja utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni dola vamizi na ghasibu.
-
Maafisa wa serikali ya Bahrain waenda kujidhalilisha Israel
Nov 18, 2020 21:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain ameongoza ujumbe wa ngazi za juu wa serikali ya Manama kuzitembelea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
-
Mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria watibua chokochoko za Israel mjini Damascus
Nov 18, 2020 21:29Mfumo wa ngao ya ulinzi wa makombora ya jeshi la Syria umefanikiwa kuzima uvamizi mpya wa utawala haramu wa Israel dhidi ya mji mkuu wa nchi hiyo ya Kiarabu, Damascus.
-
Saudi Arabia yaendeleza shughuli za siri za nyuklia chini ya mwavuli wa kutoa madai ya uongo dhidi ya Iran
Nov 18, 2020 07:17Maafisa wa utawala wa kifalme wa Sauudi Arabia wameendelea kufuata nyayo za utawala haramu wa Israel kwa kutoa tuhuma na madai yasiyo na msingi wakiitangaza miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia nchini Iran kuwa ni tishio kwa eneo la Magharibi mwa Asia.
-
Hamas na Jihad Islami zalaani hatua ya Serikali ya Ndani ya Palestina ya kushirikiana na utawala wa Kizayuni
Nov 18, 2020 04:30Harakati za Hamas na Jihad Islami za Palestina zimetoa taarifa kwa nyakati tofauti na kulaani hatua ya Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kutoa dhamana ya kuanzisha uratibu wa masuala ya usalama na utawala wa Kizayuni.
-
Shirika la Afya Duniani: Yemen inakabiliwa na mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani
Nov 18, 2020 04:11Shirika la Afya Duniani (WHO) limesisitiza kuwa mgogoro unaoikabili Yemen ni mgogoro mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa duniani na limetaka uungaji mkono wa kimataifa il kuwasaidia wananchi wa nchi hiyo.
-
Sababu na shabaha za Saudia za kushirikiana na Wazayuni kuipiga vita Ikhwanul Muslimin
Nov 18, 2020 03:16Baraza la Maulamaa Wakuu wa Saudi Arabia limetoa taarifa likidai kuwa Ikhwanul Muslimin ni la kigaidi ambalo linapigania malengo ya kichama. Aidha baraza hilo limeituhumu Ikhwanul Muslimin kuwa inazusha mifarakano, inaeneza fitna na inaendesha machafuko na vitendo vya kigaidi.
-
Oxfam: Mauzo ya silaha za G20 kwa Saudia, ni mara 3 ya msaada kwa Wayemen
Nov 17, 2020 23:02Shirika la misaada ya kibinadamu la Oxfam lenye makao makuu yake nchini Uingereza limesema nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani (G20) zimeiuzia Saudi Arabia silaha zenye thamani ya dola bilioni 17 tangu Riyadh ianzishe vita dhidi ya Yemen mwaka 2015, lakini nchi hizo wanachama wa kundi la G20 zimeipa Yemen thuluthi moja ya fedha hizo kama msaada.