-
Waziri Mkuu wa Palestina: Kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel ni maafa ya karne
Oct 26, 2020 22:58Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amelaani hatua ya nchi ya Sudan ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kuwa, maafikiano hayo yatafanya wananchi wa Palestina wazidi kuuawa.
-
HAMAS: Chokochoko za Ufaransa zimeumiza hisia za Waislamu duniani
Oct 26, 2020 08:14Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema hatua za kichochezi na kichokozi za maafisa wa serikali ya Ufaransa za kuunga mkono kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW na matukufu ya Kiislamu zimeumiza hisia na nyoyo za Waislamu kote duniani.
-
Afisa wa UN aitaka Israel imwachie huru Maher al Akhras haraka iwezekanavyo
Oct 25, 2020 23:03Ripota wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina la Israel ameutaka utawala wa Kizayuni umwachie Mpalestina Maher al Akhras haraka iwezekanavyo.
-
'Mapatano ya Saudia na Israel itakuwa zawadi Aal Saud watakayomtunukia rais ajaye wa Marekani'
Oct 25, 2020 23:02Mkuu wa shirika la ujasusi la utawala haramu wa Israel, Mossad amesema utawala wa Aal Saud unataka kumtunukia kama zawadi rais ajaye wa Marekani mapatano itakayofanya ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo wa Kizayuni.
-
Serikali ya Iraq: Hatuitambui Ikhwanul Muslimin ya Iraq kuwa ni kundi la kigaidi
Oct 25, 2020 23:01Msemaji wa serikali ya Iraq amesema kundi la Ikhwanul Muslimin ni sehemu ya mchakato wa kisiasa wa nchi hiyo na wala serikali hiyo haiitambui harakati hiyo kuwa ni kundi la kigaidi.
-
Al Houthi: Kuna udharura wa kuwa na msimamo mmoja dhidi ya vitendo vya kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad (saw)
Oct 25, 2020 13:14Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Wananchi wa Yemen amesema kuna udharura wa kuwepo msimamo mmoja wa Kiislamu dhidi ya vitendo vya kuwavunjia heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu.
-
Harakati za mapambano Palestina zaapa kulipiza kisasi cha mauaji ya kijana Amer
Oct 25, 2020 09:19Harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina zimetangaza kuwa zitajibu mauaji yaliyofaywa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kijana aliyekuwa na umri wa miaka 18 wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi kwa kuzidisha mapambano dhidi ya utawala huo.
-
Kutangaza uhusiano wa kawaida na Wazayuni, mapambano baina ya viongozi na nguvu za wananchi
Oct 25, 2020 07:47Tathmini ya kina ya wimbi lililozuka hivi sasa la baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu kutangaza uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni inaonesha kuwa, uamuzi wa kuutambua rasmi hadharani utawala huo pandikizi ni wa watu binafsi na hauungwi mkono na wananchi wa nchi za Kiarabu.
-
Iran yaalani shambulio la kigaidi Kabul, watu 18 wapoteza maisha
Oct 25, 2020 04:19Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana usiku alilaani shambulio la kigaidi lililotekelezwa huko Kabul mji mkuu wa Afghanistan na kutoa pole kwa serikali, wananchi na familia za wahanga wa jinai hiyo.
-
Mwalimu Mpalestina mkazi wa Ghaza achaguliwa mwalimu bora duniani
Oct 24, 2020 23:07Bi Asma Mustafa, mwalimu wa kike wa shule ya wasichana ya "Halima al Saadiyah" ya kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza huko Paletina ameshinda tunzo ya mwalimu boda duniani mwaka huu wa 2020 ijulikanayo kwa jina la AKS Education Award.