-
Muungano wa Nato unawapatia silaha magaidi huko Syria
Jan 20, 2020 04:09Wizara ya Ulinzi ya Russia imearifu kuwa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi Nato unawapatia silaha magaidi huko Syria.
-
Tahadhari ya UN kuhusu ukiukwaji wa haki za watoto vitani nchini Syria
Jan 19, 2020 23:24Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, katika muda wa miaka tisa ya vita huko Syria watoto wa kike na wa kiume wa nchi hiyo wamenyimwa haki zao za msingi na haki zao zimekiukwa pakubwa.
-
Yemen: Saudia na washirika wake wanatumia silaha za Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya raia
Jan 19, 2020 09:51Waziri Mkuu wa Serikali ya Uokovu ya Yemen amesema kuwa, muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unatumia silaha hatari zilizotengenezwa na Marekani, Uingireza na Ufaransa dhidi ya raia wa Yemen.
-
Maaskofu wa Kikatoliki wataka kutambuliwa rasmi nchi huru ya Palestina
Jan 19, 2020 07:56Maaskofu wa Ulaya, America ya Kaskazini na Afrika Kusini amezitaka nchi zao kuitambua rasmi nchi huru ya Palestina na kusisitiza udharura wa kuwapa Wapalestina haki zao zote.
-
Ugaidi, vikwazo na mauaji ya kigaidi, stratijia tatu za Magharibi dhidi ya kambi ya muqawama
Jan 19, 2020 07:27Wizara ya Fedha ya Uingereza katika hatua yake ya uhasama, imeliweka kikamilifu jina la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon katika orodha yake ya taasisi ambazo kwa mtazamo wa London ni za kigaidi.
-
Mamluki 60 wa Saudia waangamizwa katika shambulizi la Ansarullah Yemen
Jan 19, 2020 04:30Makumi ya mamluki wa Saudi Arabia wameuawa katika operesheni iliyofanywa na jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya Ansarullah huko kaskazini mwa Yemen.
-
Iraq: Hatua ya Marekani ya kujiondoa JCPOA, ndio chanzo cha mzozo Asia Magharibi
Jan 19, 2020 01:04Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq imesema kuwa hatua ya Marekani ya kujiondoa kwenye mapatano ya nyuklia mashuhuri kama JCPOA ndio sababu kuu ya ongezeko la mzozo wa hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi.
-
Kuongezeka ukosefu wa usalama wa chakula Ukanda wa Ghaza
Jan 18, 2020 23:24Tarehe 29 mwezi Dei sawa na Tarehe 19 Januari katika kalenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepewa jina la 'Siku ya Ghaza'. Katika kukaribia siku hii, Kamati ya Wananchi ya Kupambana na Mzingiro wa Ghaza imesisitiza kuwa ukosefu wa usalama wa chakula miongoni mwa wakazi wa Ukanda wa Ghaza mwaka jana wa 2019 ulifikia asilimia 70.
-
Mufti 'tipwatipwa' wa DAESH mwenye uzito wa kilo 245 atiwa nguvuni mjini Mosul, Iraq
Jan 18, 2020 10:37Vikosi vya usalama vya Iraq vimemtia nguvuni Abu Abdul Bari, mufti wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) katika mji wa Mosul, kaskazini mwa nchi hiyo. Abu Abdul Bari ni maarufu kwa utoaji fatua za kuwafanya wanawake watumwa, za ubakaji, utesaji na uangamizaji wa kimbari.
-
Saudia yaipa Washington dola milioni 500 kwa ajili ya uwepo wa askari wa US nchini humo
Jan 18, 2020 04:01Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imefichua kuwa, utawala wa Riyadh umeipa Washingon dola milioni 500, kama malipo ya kugharamia uwepo wa askari wa Marekani katika nchi hiyo ya Kiarabu.