Muungano wa Nato unawapatia silaha magaidi huko Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58630-muungano_wa_nato_unawapatia_silaha_magaidi_huko_syria
Wizara ya Ulinzi ya Russia imearifu kuwa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi Nato unawapatia silaha magaidi huko Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 20, 2020 04:09 UTC
  • Muungano wa Nato unawapatia silaha magaidi huko Syria

Wizara ya Ulinzi ya Russia imearifu kuwa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi Nato unawapatia silaha magaidi huko Syria.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imeeleza kuwa kuanzia Januari 16 hadi sasa; wanajeshi 47 wa Syria na raia 51 wameuliwa katika mashambulizi ya magaidi katika maeneo mbalimbali mkoani Idlib kaskazini mwa SYria. Imeongeza kuwa magaidi hao wanatumia silaha za muungano wa Nato kuwaulia wananchi wa Syria. 

Oparesheni ya jeshi la Syria ya kuikomboa Idlib  

Jeshi la Syria hadi sasa limenasa maghala kadhaa ya silaha na zana za kijeshi katika maeneo tofauti nchini humo zilizoundwa Israel na katika nchi nyingine za Magharibi ikiwemo Marekani.  

Mkoa wa Idlib ni ngome ya mwisho ya magaidi huko Syria. Syria ilitumbukia katika hali ya mgogoro mwaka 2011 kufuatia uvamizi mkubwa wa makundi ya kigaidi kwa uungaji mkono wa hali na mali wa Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wake kwa lengo la kubadili mlingano katika eneo kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni.  

Syria iliomba msaada wa Iran na Russia ili kupambana na makundi ya kigaidi baada ya kukumbwa na uvamizi huo tajwa. Hivi sasa magaidi hao wanaendelea kusambaratishwa huko Syria siku baada ya siku.