-
Onyo kali la Muqtada al-Sadr na kuwa pamoja makundi yote ya muqawama nchini Iraq dhidi ya Marekani
Jan 08, 2020 21:45Moja ya matokeo muhimu ya jinai ya serikali ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandes na watu wanane waliokuwa wamefuatana nao ni kujitokeza hali ya umoja baina ya makundi ya muqawama nchini Iraq dhidi ya Marekani.
-
Muungano wa Marekani wahamisha makao yake makuu kutoka Iraq hadi Kuwait
Jan 07, 2020 23:21Muungano eti wa kupambana na kundi la Daesh unaoongozwa na Marekani umehamisha makao yake makuu kutoka Iraq na kuyapeleka Kuwait kufuatia mauaji ya Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hashdul Shaabi Abu Mahdi al Muhandes, na sisitizo la Iran la kulipiza kisasi mauaji hayo ya kigaidi yaliyofanywa na Marekani.
-
Putin atembelea Syria na kukutana Assad, atembelea mitaa ya Damascus
Jan 07, 2020 23:19Rais Vladimir Putin wa Russia jana aliwasili Damascus mji mkuu wa Syria na kukutana na Rais wa nchi hiyo, Bashar Assad.
-
Middle East Eye: Saudia inazidisha mashaka ya Waislamu wa Rohingya
Jan 07, 2020 23:18Kituo cha habari cha Middle East Eye kimeripoti kuwa, Saudi Arabia inazidisha mashaka na masaibu ya Waislamu wa jamii ya Rohingya huko Myanmar kwa kuwasaka, kuwakamata na kuwafukuza Warohingya wanaofanya kazi nchini humo.
-
Netanyahu apatwa na kiwewe cha jibu kali la muuqawama kufuatia jinai dhidi ya Luteni Soleimani
Jan 07, 2020 01:30Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala Haramu wa Kizayuni wa Israel, amelegeza msimamo kunako msimamo wake wa awali wa kuunga mkono jinai ya kigaidi iliyofanywa na Marekani ya kuwaua shahidi viongozi wa mrengo wa muqawama, ambapo sasa amesema kuwa Israel haikuhusika katika shambulizi hilo la Marekani katika uwanja wa ndege wa Baghdad, Iraq.
-
Harakati ya Hizbullah ya Iraq yampa onyo kali Rais Donald Trump wa Marekani
Jan 07, 2020 01:11Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Iraq imemuonya Rais Donald Trump wa Marekani kwamba iwapo ataiwekea vikwazo nchi hiyo, basi harakati hiyo itazuia usafirishaji mafuta ya kwenda soko la nchi hiyo.
-
Answarullah ya Yemen: Damu ya Jenerali Qasem Soleimani imeainisha njia ya kuhitimisha uwepo wa Marekani katika eneo
Jan 06, 2020 10:07Salim Al-Mughlis, Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Wananchi ya Answarullah ya nchini Yemen amesema kuwa shahidi Qassem Soleimani ameainisha njia ya kuhitimisha uwepo wa Marekani katika eneo hili.
-
Sababu na taathira za mauaji ya kigaidi ya kamanda Qassem Soleimani kwa mtazamo wa Sayyid Hassan Nasrullah
Jan 06, 2020 07:42Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah amebainisha sababu, matokeo na taathira za jinai iliyofanywa na Marekani, ya kumuua kigaidi kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Naibu Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq Abu Mahdi Al-Muhandis pamoja na wanamuqawama wengine kadhaa; na akasisitiza kwamba, jinai hiyo ya Washington itapelekea kuanza historia mpya Asia Magharibi.
-
Waziri Mkuu wa Iraq: Soleimani alikuwa mgeni wangu rasmi aliyekuja na ujumbe wa Saudi Arabia
Jan 06, 2020 04:43Kaimu Waziri Mkuu wa Iraq, Adel Abdul Mahdi amesema kuwa, Luteni Jenerali Qassem Soleimani alielekea nchini Iraq akiwa mgeni rasmi wa serikali na alikwenda na ujumbe wa Saudi Arabia kuhusu mazungumzo.
-
Hizbullah: Luteni Jenerali Qassim Soleimani alikuwa kamanda wa ulimwengu wa Kiislamu
Jan 05, 2020 23:20Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani hakuwa kamanda wa Iran tu bali alikuwa kamanda wa ulimwengu wa Kiislamu na kambi ya muqawama dhidi ya wavamizi na mabeberu wa dunia.