-
Muqtada al-Sadr: Ubalozi na kambi zote za kijeshi za Marekani nchini Iraq zipigwe kufuli mara moja
Jan 05, 2020 12:56Muqtada al-Sadr, Kiongozi wa Harakati ya Al-Sadr ya nchini Iraq ametoa ujumbe leo kwenda kwa spika wa bunge akitaka kupigwa kufuli ubalozi wa Marekani na kambi zake za kijeshi nchini humo.
-
Bunge la Iraq lapitisha mpango wa kuwatimua askari wa jeshi la Marekani walioko nchini humo + Video
Jan 05, 2020 12:48Bunge la Iraq limepiga kura na kupitisha mpango uliopendekezwa na wabunge wa kuhitimisha makubaliano ya kijeshi yaliyofikiwa kati ya nchi hiyo na Marekani na kuwataka wanajeshi wa Marekani waondoke nchini humo.
-
Nasrullah: Siku ya kuuawa shahidi Kamanda Soleimani, mwanzo wa historia mpya Mashariki ya Kati + Video
Jan 05, 2020 12:26Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tarehe 3 Januari 2020 ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, ni mwanzo wa historia mpya katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Wapalestina: Sehemu kubwa ya juhudi za Shahidi Soleimani zilihusu ukombozi wa Palestina
Jan 04, 2020 04:15Brigedi za shahidi Izzuddin-al Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alielekeza sehemu kubwa ya juhudi zake kwa ajili ya kuutokomeza na kuuangamiza utawala wa Kizayuni na kuhitimisha kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
-
Shughuli ya kuuaga mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani yafanyika Kadhimain, Iraq
Jan 04, 2020 03:46Shughuli maalumu ya maombolezo ya kuuaga mwili wa shahidi Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) pamoja na wanamapambano wenzake waliouawa shahidi pamoja naye imefanyika katika mji wa Kadhimain nchini Iraq.
-
Wairaqi walaani vikali kuuawa Qassem Soleimani na Abu Mahdi
Jan 03, 2020 23:20Shakhasia mbali mbali wa kisiasa na kidini nchini Iraq wamelaani vikali hujuma ya kigaidi ya Mareknai ambayo imepelekea Meja Jenerali Qassem Suleimani na Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq (Al Hashd al Shaabi) Abu Mahdi la Muhandis kuuawa shahidi.
-
Sayyid Nasrullah: Vikosi vya Muqawama kote duniani kujibu mapigo ya kuuawa shahidi Soleimani
Jan 03, 2020 10:25Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema vikosi vya wanamuqawama kote duniani vina jukumu la kuwaadhibu wale waliohusika na mauaji ya kikatili ya Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Meja Jenerali Qassem Solaimani.
-
Netanyahu anatafuta kinga ya kutopandishwa kizimbani
Jan 02, 2020 23:20Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza kuwa ametuma ombi kwa bunge la utawala huo, Knesset, akitaka kinga ya kutofikishwa kizimbani kuhusiana na mashtaka yanayomkabili.
-
Waziri wa Ulinzi wa Marekani atoa vitisho kwa Iraq kwamba nchi yake itafanya mashambulizi zaidi dhidi ya taifa hilo
Jan 02, 2020 13:52Waziri wa Ulinzi wa Marekani sambamba na kuituhumu Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi kwa kile alichokidai kuwa ni hatua za kichochezi, ametishia kuzidisha mashambulizi nchini Iraq.
-
Sheikh Issa Qassim: Shambulio la Marekani dhidi ya al-Hashd al-Shaabi ni hujuma dhidi ya Umma wa Kiislamu
Jan 02, 2020 04:38Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Bahrain amelaani shambulio la anga la Marekani dhidi ya ngome za Harakati ya Wananchi ya al-Hashd al-Shaabi nchini Iraq na kusema kuwa, ni wajibu kukabiliana na hujuma kama hizo.