-
Abdul-Malik al-Houthi; "imani" siri ya ushindi wa Yemen
Dec 19, 2019 21:38Abdul-Malik al-Houthi, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema katika hotuba yake kupitia video aliyoitoa mbele ya Maulamaa na maafisa wa Yemen kwamba, imani ndio siri ya mafanikio ya Wayamen katika vita vya miaka mitano na muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia.
-
Sisitizo la Waziri Mkuu wa Malaysia la kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu
Dec 19, 2019 07:37Waziri Mkuu wa Malaysia amesisitiza katika Mkutano wa Viongozi wa nchi za Kiislamu wa "Kuala Lumpur 2019" juu ya udharura wa kukabiliana na kampeni za chuki dhidi ya Uislamu.
-
Nchi za Kiarabu, miaka 9 baada ya kujichoma moto Bouazizi
Dec 19, 2019 04:42Tarehe 17 Disemba miaka 9 iliyopita kijana muuza mboga wa Tunisia, Tariq Mohamed Bouazizi alijiteketeza kwa moto akilalamikia kitendo cha kudhalilishwa na polisi wa nchi hiyo. Tukio lilikuwa cheche ya harakati ya mapinduzi ya wananchi wa Tunisia na katika nchi nyingine za Kiarabu kama Misri, Libya, Yemen na Bahrain dhidi ya watawala dhalimu na vibaraka wa nchi za Magharibi.
-
Makumi ya askari wa Ufaransa wajiunga na makundi ya kigaidi Iraq na Syria
Dec 19, 2019 00:36Kituo cha Kuchunguza Ugaidi cha Ufaransa kimetangaza kuwa wanajeshi 30 wa nchi hiyo wamejiunga na makundi ya kigaidi katika nchi za Syria na Iraq.
-
Walowezi wa Kizayuni wavamia tena Msikiti Mtakatifu wa al-Aqswa
Dec 18, 2019 08:11Walowezi wa Kizayuni leo wameuvamia tena Msikiti wa al-Aqswa huko Palestina wakisaidiwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel na kuuvunjia heshima msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
-
Al-Wifaq: Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaendelea kufanyika katika magereza ya Bahrain
Dec 18, 2019 04:32Jumuiya ya Kitaifa ya Kiislamu ya al Wifaq ya Bahrain imetangaza katika ripoti yake kwamba, utawala wa kifamilia wa nchi hiyo wa Aal Khalifa unaendelea kukiuka pakubwa haki za wafungwa katika magereza ya nchi hiyo.
-
Saudia yaongoza duniani kwa ufanyaji israfu kubwa katika chakula
Dec 18, 2019 00:41Saudi Arabia inaongoza kati ya nchi 25 duniani zinazomwaga na kutupa jaani kiwango kikubwa zaidi cha chakula.
-
Kuwait, mwenyeji wa mkutano wa shirika la NATO
Dec 17, 2019 22:08Ujumbe wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) ukiongozwa na Katibu Mkuu wa shirika hilo, Jens Stoltenberg umekuwa nchini Kuwait ambako umeshiriki katika kikao cha masuala ya usalama na maafisa wa baadhi ya nchi za Kiarabu.
-
Qatar: Iran ni jirani muhimu kwa nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi
Dec 17, 2019 09:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Muhammad bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni jirani muhimu kwa nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon aunga mkono misimamo ya Hizbullah
Dec 17, 2019 09:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon Gebran Bassil ameunga mkono misimamo ya harakati ya muqawama ya Hizbullah katika uga wa kisiasa na kijeshi wa nchi hiyo.