-
Ulaya kuitambua rasmi Palestina ni hatua iliyochukuliwa kwa kuchelewa au ni ubadilishaji wa mkakati tu?
Jul 31, 2025 23:15Siku chache baada ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kutangaza kuwa atalitambua rasmi taifa la Palestina katika Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, serikali ya Uingereza nayo pia imesisitiza kuwa hivi karibuni itaitambua nchi ya Palestina.
-
Canada kuitambua rasmi nchi ya Palestina mwezi Septemba mwaka huu
Jul 31, 2025 08:51Markk Carney Waziri Mkuu wa Canada ametangaza kuwa nchi hiyo imepanga kuitambua rasmi nchi ya Palestina katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu.
-
UNICEF: Watoto 80,000 wako katika hatari kubwa ya kipindupindu Magharibi na Katikati mwa Afrika
Jul 31, 2025 08:41Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeripoti kuwa, takriban watoto 80,000 wako katika hatari kubwa ya kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu wakati msimu wa mvua utakapoanza katika maeneo ya Magharibi na Katikati mwa Afrika.
-
Guterres atoa wito wa ulimwengu ambako "hakuna mtu anayeuzwa au kununuliwa"
Jul 31, 2025 04:03Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito wa kuwepo ulimwengu "ambapo hakuna mtu anayenunuliwa, kuuzwa au kunyonywa," akisisitiza udharura wa kuchukuliwa hatua za pamoja za kusaidia waathiriwa wa biashara haramu ya binadamu na kuwawajibisha wahalifu.
-
Kwa nini kizazi kipya cha Wamarekani hakiipendi tena Israel?
Jul 31, 2025 02:09Kwa miongo kadhaa, kuiunga mkono Israel nchini Marekani haukuwa tu msimamo wa kisiasa bali pia sehemu ya utambulisho wa taifa kwa raia wengi. Katika duru za kisiasa, vyombo vya habari, na taasisi za elimu ya juu, uaminifu kwa Israel ulionekana kama thamani ya pamoja ya Wamarekani. Lakini hali hiyo sasa imebadilika, hasa miongoni mwa vijana wa kizazi kipya.
-
Kongamano la UN lataka kutambuliwa rasmi taifa la Palestina, lapinga mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza
Jul 30, 2025 09:19Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa umezihimiza nchi zote kutambuliwa Palestina kama taifa, na kulaani vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza vilivyoanza Oktoba 2023.
-
Japan yafunga kinu cha nyuklia cha Fukushima baada ya tetemeko la ardhi nchini Russia
Jul 30, 2025 09:14Japan leo Jumatano imewahamisha wafanyakazi wote wa kinu cha nyuklia cha Fukushima mashariki mwa nchi hiyo ikihofia athari za tetemeko kubwa la ardhi lililopiga pwani ya Rasi ya Kamchatka mashariki mwa Russia mapema leo asubuhi.
-
Wagiriki wawazuia watalii wa Israel kuingia katika fukwe za Ugiriki
Jul 30, 2025 04:17Kufuatia mauaji ya watu wa Gaza na kuzuiwa misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo; wananchi wa Ugiriki hawawaruhusu tene watalii wa Israel kuingia katika visiwa vya nchi yao, suala ambalo limesababisha mapigano kati yao na polisi wa Ugiriki.
-
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 8.7 laikumba pwani ya Russia, tahadhari ya Tsunami yatolewa
Jul 29, 2025 23:41Tahadhari za kuzuka Tsunami zimetolewa katika nchi kadhaa baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 8.7 kulikumba eneo la mashariki ya Russia la Peninsula ya Kamchatka.
-
Uholanzi yawazuia kuingia nchini Ben-Gvir na Smotrich kwa kuchochea machafuko na maangamizi ya kizazi Ghaza
Jul 29, 2025 23:24Uholanzi imewataja mawaziri wa Israeli Itamar Ben-Gvir na Bezalel Smotrich kuwa watu wasiokubalika na hivyo imewapiga marufuku kuingia nchini humo kutokana na vitendo vyao vya kuwachochea walowezi wa Kizayuni kuendesha ghasia na vitendo vya mabavu dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na maangamizi ya kizazi katika Ukanda wa Gaza.