Uchunguzi wa maoni: Theluthi mbili ya Wafaransa wanaunga mkono kujiuzulu Macron
https://parstoday.ir/sw/news/world-i130428-uchunguzi_wa_maoni_theluthi_mbili_ya_wafaransa_wanaunga_mkono_kujiuzulu_macron
Matokeo ya uchunguzi wa maoni yaliyotolewa siku tatu kabla ya uwezekano wa kuanguka serikali ya Waziri Mkuu wa Ufaransa, François Bayrou, yanaonyesha kuwa karibu theluthi mbili ya Wafaransa, ambao imani yao kwa viongozi wa sasa wa kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo imepungua, wanataka Rais Emmanuel Macron ajiuzulu.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Sep 05, 2025 03:34 UTC
  • Uchunguzi wa maoni: Theluthi mbili ya Wafaransa wanaunga mkono kujiuzulu Macron

Matokeo ya uchunguzi wa maoni yaliyotolewa siku tatu kabla ya uwezekano wa kuanguka serikali ya Waziri Mkuu wa Ufaransa, François Bayrou, yanaonyesha kuwa karibu theluthi mbili ya Wafaransa, ambao imani yao kwa viongozi wa sasa wa kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo imepungua, wanataka Rais Emmanuel Macron ajiuzulu.

Kwa mujibu wa kura ya maoni iliyofanywa na Odoxa kwa ajili ya gazeti la kihafidhina la Le Figaro, asilimia 64 ya Wafaransa wanataka rais mpya na uchaguzi wa mapema wa rais, badala ya kumteua waziri mkuu wa tano katika muda wa chini ya miaka miwili. Asilimia 56 kati yao wanatoa wito wa kufanyika uchaguzi wa mapema wa wabunge ili kutatua mgogoro huo.

Katika kura nyingine ya maoni iliyofanywa na Verian kwa ajili ya Jarida la Le Figaro, 15% tu ya Wafaransa ndio walioonyesha imani kwa rais Macron, jambo linaloakisi kushuka kwa kasi na kusiko na kifani kwa umaarufu wa kiongozi huyo ikilinganishwa na Julai 2025.

Siku chache kabla ya Bunge la Taifa la Ufaransa kupiga kura, mustakabali wa Waziri Mkuu wa Ufaransa, François Bayrou, unaonekana kuwa mbaya baada ya upinzani kutangaza kuwa hautapiga kura ya kuwa na imani naye kutokana na udharura wa kupunguza deni.