-
Wamalaysia waandamana na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua kukomesha mauaji ya Kimbari ya Israel Gaza
Aug 11, 2025 23:08Maelfu ya raia nchini Malaysia wameandamana ambapo mbali na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina wametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka na za maana kukomesha mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
-
Australia nayo kuitambua rasmi Palestina katika mkutano ujao wa UNGA
Aug 11, 2025 23:06Serikali ya Australia nayo imetangaza kuwa, inatarajia kuitambua rasmi Palestina mwezi ujao wa Septemba.
-
Korea Kaskazini: ‘Tutajibu’ mazoezi ya kijeshi ya Korea Kusini na Marekani
Aug 11, 2025 23:05Korea Kaskazini imekosea mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya hasimu wake Korea Kusini na Marekani na kuyataja kama "uchochezi wa moja kwa moja wa kijeshi" na kuonya kuwa itachukua hatua za kujibu.
-
Ukiondoa US, wanachama 4 wa kudumu wa UNSC wamelaani mpango wa Israel kuhusu Ghaza
Aug 11, 2025 08:22Nchi nne kati ya tano, wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimelaani mpango wa utawala wa kizayuni wa Israel kuukalia kikamilifu Ukanda wa Ghaza. Ni Marekani pekee ndiyo iliyotetea uamuzi huo wa utawala wa kizayuni wakati wa mkutano wa dharura wa baraza hilo uliofanyika jana Jumapili.
-
Israel yalaaniwa vikali kila pembe ya dunia kwa mauaji ya wanahabari 5 Wapalestina Ghaza
Aug 11, 2025 07:18Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu na jumuiya mbalimbali za waandishi wa habari duniani zimelaani vikali mauaji ya kigaidi ya wanahabari watano Wapalestina yaliyofanywa na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.
-
Watu zaidi ya 530 watiwa nguvuni London kwa kuiunga mkono Palestina
Aug 11, 2025 05:36Polisi ya London imetangaza kuwa jumla ya waandamanaji 532 wametiwa mbaroni wakati wa maandamano ya kuunga mkono kundi linalojulikana kwa jina la Palestine Action Group linalowatetea Wapalestina.
-
Ripota wa UN: Israel inajaribu kuua ukweli kwa kuwaua waandishi habari, itashindwa
Aug 10, 2025 23:44Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa maoni na kujieleza, Irene Khan, amesema kuwa jeshi la Israel linataka "kuua ukweli" kwa kunyamazisha kila sauti inayosimulia kile kinachotokea katika Ukanda wa Gaza, akisisitiza kwamba mwandishi wa televisheni ya Al Jazeera, Anas Al-Sharif aliyeuawa na jeshi la Israel, alikuwa "mwandishi wa habari jasiri" ambaye aliendelea na kazi yake licha ya vitisho vya moja kwa moja kwa maisha yake.
-
Save the Children: "Watoto wa Gaza, njaa hadi mauti"
Aug 10, 2025 23:12Shirika la kimataifa la "Save the Children" limetangaza kuwa, mzingiro wa Israel umewaweka watoto katika Gaza kwenye njaa mbaya, na hadi sasa watoto 100 wamekufa kutokana na njaa.
-
Uko wapi mpaka kati ya ukosoaji dhidi ya Israel na chuki dhidi ya Wayahudi? Trump na mradi wa kudhibiti vyuo vikuu
Aug 10, 2025 23:10Kufuatia kushamiri maandamano ya wanafunzi katika vyuo vikuu vya Marekani mwaka 2024, ambayo yalifanyika hasa kwa ajili ya kuunga mkono na kuwatetea watu wa Ukanda wa Gaza na kupinga misaada ya Washington kwa ukatili wa Israel, serikali ya sasa ya Marekani kwa mara nyingine tena imechukua hatua yenye utata dhidi ya vyuo vikuu vya nchi hiyo.
-
'Tuambie jinsi alivyokufa': MO Salah akosoa heshima ya UEFA kwa 'Pele wa Palestina'
Aug 10, 2025 10:48Mshambuliaji wa timu ya soka ya Liverpool, Mohamed Salah amekosoa hatua ya Muungano wa Vyama vya Soka vya Ulaya UEFA ya kumuenzi Suleiman Al-Obeid, anayejulikana kama "Pele wa Palestina," baada ya bodi inayosimamia soka ya Ulaya kutoelezea mazingira ya kifo chake wiki hii.