Watu zaidi ya 530 watiwa nguvuni London kwa kuiunga mkono Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129402
Polisi ya London imetangaza kuwa jumla ya waandamanaji 532 wametiwa mbaroni wakati wa maandamano ya kuunga mkono kundi linalojulikana kwa jina la Palestine Action Group linalowatetea Wapalestina.
(last modified 2025-08-11T09:06:42+00:00 )
Aug 11, 2025 09:06 UTC
  • Watu zaidi ya 530 watiwa nguvuni London kwa kuiunga mkono Palestina

Polisi ya London imetangaza kuwa jumla ya waandamanaji 532 wametiwa mbaroni wakati wa maandamano ya kuunga mkono kundi linalojulikana kwa jina la Palestine Action Group linalowatetea Wapalestina.

Polisi ya London imeeleza kwamba waandamanaji 522 wametiwa nguvuni kwa kitendo chao cha kuonyesha mabango yenye maandishi ya kuliunga mkono kundi la "Palestinian Action".

Polisi ya Uingereza imedai kuwa kundi hilo limekiuka kifungu cha 13 cha Sheria ya Ugaidi ya nchi hiyo ya mwaka 2000.  

Taraifa ya Polisi ya Uingereza imeeleza kuwa: Polisi imewakamata watu wengine 10, wakiwemo sita kwa kuwashambulia askari, mmoja kwa kumzuia afisa polisi wakati wa kazi, wawili kwa makosa ya kukiuka sheria za umma na mmoja kwa kufanya uhalifu wa kibaguzi. 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: Watu 18 bado wanashikiliwa korokoroni lakini wanatazamiwa kuachiwa huru kwa dhamana saa chache zijazo. 

Hatua hizo za Polisi ya Uingereza zimetajwa kuwa zimechochewa na lobi za Wazayuni zinazopiga vita kundi au jumuiya yoyote inayowatetea Wapalestina na kulaani mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza.