Nov 03, 2025 02:20 UTC
  • Jumatatu, 03 Novemba, 2025

Leo ni Jumatatu tarehe 12 Mfunguo Nane Jamadil Awwal 1447 Hijria inayosadifiana na tarehe 3 Novemba 2025.

Katika siku kama ya leo miaka 490 iliyopita alifariki dunia msomi mkubwa wa Kiislamu Ibn Tulun Dimashqi, aliyekuwa faqihi, mwanafasihi na mwanahistoria huko mjini Damascus, Syria.

Ibn Tulun alizaliwa mwaka 880 Hijiria mjini Damascus na katika umri wake wote alifanya jitihada kubwa za utafiti, kufundisha na kuandika vitabu katika taaluma mbalimbali.

Ibn Tulun Dimashqi ameandika vitabu vingi vya thamani kuhusiana na historia ya Kiislamu na pia katika uwanja wa tafsiri ya Qur'ani Tukufu, Hadithi, lugha, tiba na irfani. Kitabu cha 'as-Safiinatu al-Tuluuniyyah' ni miongoni mwa athari za mwanazuoni huyo. 

Siku kama ya leo miaka 121 iliyopita, nchi ya Panama ilifanikiwa kujipatia uhuru wake kutoka Colombia na siku hii huadhimishwa nchini humo kama siku ya taifa. Ardhi ya Panama iligunduliwa na kukaliwa kwa mabavu na Wahispania mnamo mwaka 1501. Panama ilikaliwa kwa mabavu na Colombia mwaka 1821 Miladia na tangu wakati huo wananchi wa nchi hiyo walianzisha mapambano dhidi ya wavamizi wa Colombia. Mapambano hayo ya wananchi yalishadidi zaidi baada ya kuwasilishwa mpango wa mfereji wa Panama. Mwaka 1903, Panama ikafanikiwa kujitenga na Colombia na kujitawala.

Miaka 68 iliyopita muwafaka na siku kama hii ya leo, wakati wa kujiri mashambulio ya askari wa utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Misri, wanajeshi wa utawala huo waliuvamia mji wa Khan Yunis katika Ukanda wa Gaza huko Palestina na kuwaua kwa umati wakazi wa mji huo. Baada ya kuukalia kwa mabavu mji huo, askari hao waliwanyonga askari 25 wa Kimisri. Unyama wa askari hao haukuishia hapo, kwani waliishambulia hospitali ya mkoa mjini Khan Yunis na kuwaua kwa umati wauguzi, madaktari na wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo. Watu wapatao 275 waliuawa katika mashambulio hayo.   

Na siku kama ya leo miaka 29 iliyopita, alifariki dunia Jenerali Jean-Bedel Bokassa dikteta wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Bokassa alichukua madaraka mwaka 1921 kupitia mapinduzi ya kijeshi, baada ya kuiondoa madarakani serikali ya Rais David Dacko kwa uungaji mkono wa Ufaransa. Katika miaka 14 ya utawala wake, kiongozi huyo alitenda jinai na mauaji mbalimbali na kujilimbikizia mali nyingi.