-
Uingereza yailalamikia Israel kwa kuwakamata, kuwadhalilisha na kuwatimua wabunge wake
Apr 07, 2025 03:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza ameulaumu utawala wa Kizayuni Israel kwa kuwazuia kuingia, kuwakamata na kisha kuwatimua wabunge wawili wa chama tawala cha nchi hiyo cha Leba katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.
-
Trump atishia kuzikatia misaada Misri na Jordan na kutaka makubaliano ya kusitisha vita Ghaza yafutwe
Feb 11, 2025 06:52Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaweza akafikiria kusitisha msaada kwa Jordan na Misri ikiwa zitakataa kuwapokea Wapalestina, baada ya kutekeleza mpango wake wa kuwahamaisha kwa nguvu wananchi hao katika ardhi yao ya Ukanda wa Ghaza ili kulihodhi na kulimiliki eneo hilo lililowekewa mzingiro.
-
Marekani yasimamisha misaada mipya ya fedha nje ya nchi, Israel na Misri hazimo
Jan 25, 2025 06:12Serikali mpya ya Marekani imetangaza kuwa inasitisha takribani ufadhili wote mpya wa msaada wa fedha wa nje ya nchi isipokuwa kwa washirika wake wawili ambao ni utawala wa Kizayuni wa Israel na Misri. Haijafahamika wazi kama uamuzi huo utaihusu pia Ukraine au la.
-
Iran: HAMAS ingali hai, itaendeleza njia yake kwa nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla
Oct 20, 2024 07:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS iko hai na itaendelea kufuata njia yake hiyo hiyo kwa nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla licha ya kuuawa shahidi kiongozi wake Yahya Sinwar.
-
Sadiq Khan: Usalama umeimarishwa katika misikiti ya London
Aug 15, 2024 14:15Meya wa jiji la London ametangaza kuongezwa hatua za usalama katika mji huo ikiwa ni pamoja na mafunzo katika misikiti katika mji mkuu huo wa Uingereza.
-
Upinzani mkubwa dhidi ya uingiliaji wa London katika masuala ya Waislamu
Jun 03, 2023 01:30Idadi kubwa ya Waislamu wamekusanyika mbele ya Kituo cha Kiislamu mjini London wakipinga uingiliaji wa serikali ya Uingereza katika masuala ya Waislamu na kuwekewa mkurugenzi asiye Muislamu kusimamia masuala ya kituo hicho cha ibada.
-
Mtikisiko wa baada ya kifo cha Malkia Elizabeth: Nchi za Caribbean zaidai London fidia ya kipindi cha ukoloni na utumwa
Sep 09, 2022 12:17Wanasiasa na wanaharakati katika makoloni ya zamani ya Uingereza katika eneo la Caribbean, wamesisitiza tena ombi lao La kuondoka chini ya utawala wa familia ya kifalme ya Uingereza na kupewa fidia ya ukoloni na kipindi cha utumwa.
-
Balozi wa Israel akimbilia usalama wake kutoka Chuo cha Uchumi cha London
Nov 11, 2021 08:50Malalamiko na hasira ya wanachuo na waungaji mkono wa taifa la Palestina katika Chuo cha Masuala ya Uchumi cha London imepelekea balozi wa utawala haramu wa Israel nchini Uingereza kukimbilia usalama wake kutoka kwenye chuo hicho.
-
Maelfu ya watu wasio na makazi wamefariki dunia mjini London
Dec 16, 2019 12:12Vyombo vya habari nchini Uingereza vimetangaza habari ya kufariki dunia maelfu ya watu wasio na makazi mjini London, mji mkuu wa nchi hiyo.
-
NATO na changamoto zinazoikabili wakati inaadhimisha mwaka wa 70 wa kuasisiwa kwake
Dec 04, 2019 08:12Nchi wanachama wa shirika la kijeshi la NATO zinakutana mjini London, Uingereza katika mkutano unaoadhimisha mwaka wa 70 tangu kuasisiwa shirika hilo la kijeshi, huku tofauti kubwa na changamoto za mivutano zilizopo ambazo hazijawahi kushuhudiwa, zikiuweka mashakani mustakabali wake.