Ziara ya Gharibabadi nchini Saudi Arabia inalenga kuimarisha ushirikiano
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i132864-ziara_ya_gharibabadi_nchini_saudi_arabia_inalenga_kuimarisha_ushirikiano
Naibu Waziri wa Sheria na Masuala ya Kimataifa wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesafiri hadi Saudi Arabia kwa ajenda ya kuimarisha ushirikiano.
(last modified 2025-11-06T10:43:43+00:00 )
Nov 06, 2025 10:31 UTC
  • Ziara ya Gharibabadi nchini Saudi Arabia inalenga kuimarisha ushirikiano
    Ziara ya Gharibabadi nchini Saudi Arabia inalenga kuimarisha ushirikiano

Naibu Waziri wa Sheria na Masuala ya Kimataifa wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesafiri hadi Saudi Arabia kwa ajenda ya kuimarisha ushirikiano.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya kimataifa na kisheria, Kazem Gharibabadi, amesisitiza umuhimu wa kistratejia wa kurejeshwa kwa uhusiano na Saudi Arabia, akisema kuwa kuimarika kwa mahusiano ya kirafiki kati ya Tehran na Riyadh ni kwa faida za pande mbili na pia ni nguvu muhimu ya kuimarisha uthabiti wa eneo na amani ya kimataifa.

Gharibabadi ametoa kauli hizo kupitia ukurasa wake wa X, kufuatia ziara nchini Saudi Arabia iliyolenga kuendeleza ushirikiano na uratibu kati ya mataifa hayo mawili yenye uzito mkubwa katika eneo.

Naibu waziri huyo amesisitiza kuwa Iran na Saudi Arabia, ambazo zina maslahi mengi ya pamoja na zinaheshimiana, ziko katika nafasi nzuri kuhudumia manufaa ya watu wao na kusukuma mbele amani ya kikanda.

Amefafanua kuhusu mazungumzo yake na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Abdulrahman al-Rassi.

Amesema mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano ndani ya taasisi za kimataifa, za kikanda na kimataifa za pande nyingi, pamoja na kusukuma mbele maeneo muhimu kama haki za binadamu na ushirikiano wa kisheria na kimahakama.