Save the Children: "Watoto wa Gaza, njaa hadi mauti"
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129390
Shirika la kimataifa la "Save the Children" limetangaza kuwa, mzingiro wa Israel umewaweka watoto katika Gaza kwenye njaa mbaya, na hadi sasa watoto 100 wamekufa kutokana na njaa.
(last modified 2025-08-11T05:06:23+00:00 )
Aug 11, 2025 02:42 UTC
  • Save the Children:

Shirika la kimataifa la "Save the Children" limetangaza kuwa, mzingiro wa Israel umewaweka watoto katika Gaza kwenye njaa mbaya, na hadi sasa watoto 100 wamekufa kutokana na njaa.

Shirika la Save the Children limeeleza kuwa, baa la njaa huko Gaza ni mgogoro unaosababishwa na binadamu na unaweza kuzuilika kabisa.

Taarifa ya shirika hilo pia iliongeza kuwa, misaada ya kudondosha kwa ndege ni njia hatari na haikidhi mahitaji ya watu ambao kwa wakati mmoja wako chini ya mabomu na mzingiro chakula.

Kwa upande wake timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa imelaani hatua ya Israel ya kuzidisha kampeni yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza na kuitaka jamii ya kimataifa kukomesha "ushiriki" wake katika uhalifu wa Israel na kukabiliana na ukatili wa utawala huo.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema: Zaidi ya watu 500,000, robo ya wakazi wa Gaza, wanakabiliwa na njaa, wakati wengine waliobaki wanakumbana na viwango tofauti vya njaa. Wameongeza kuwa watoto 320,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wa Ukanda wa Gaza wako katika hatari ya utapiamlo mkali.

Hali ya mambo kwa upande wa afya na maisha imezorota sana huku mfumo wa afya ukisambaratika kikamilifu huko Gaza. 

Licha ya malori yaliyobeba misaada kurundikana katika lango la Ukanda wa Gaza, lakini utawala ghasibu wa Israel unaendelea kuzuia kuingia malori hayo huko Gaza nje ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.