Ramzy Abou Ibrahim aapa kulitetea taifa lake la Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i129612
Ramzy Abou Ibrahim, mkuu wa Jumuiya ya Wapalestina nchini Nigeria, amesema kuwa, Wapalestina kamwe hawatasalimisha ardhi yao licha ya uvamizi wa Israel, huku wakitetea kwa dhati haki ya Hizbullah ya kumiliki wa silaha dhidi ya vikosi vinavyokalia kwa mabavu.
(last modified 2025-08-17T04:22:19+00:00 )
Aug 17, 2025 02:26 UTC
  • Ramzy Abou Ibrahim aapa kulitetea taifa lake la Palestina

Ramzy Abou Ibrahim, mkuu wa Jumuiya ya Wapalestina nchini Nigeria, amesema kuwa, Wapalestina kamwe hawatasalimisha ardhi yao licha ya uvamizi wa Israel, huku wakitetea kwa dhati haki ya Hizbullah ya kumiliki wa silaha dhidi ya vikosi vinavyokalia kwa mabavu.

Mwanaharakati huyo amesema hayo katika mahojiano la Shirika la Habari na IranPress na kusisitiza udharura wa kusimama kidete na kukabiliana na adui mvamizi.

"Netanyahu anataka kuwaua Wapalestina wote au kutuhamisha hadi Sudan Kusini. Ujumbe wangu: Tutakufa kabla ya kuondoka katika nchi yetu."

Ulimwengu unaona mbinu za njaa za utawala wa kizayuni wa Israel [huko Gaza], lakini wanawaua waandishi wa habari ili kuficha ugaidi wao."

"Wapigania uhuru kama Hizbollah ya Lebanon wana kila haki ya kutumia silaha chini ya sheria za kimataifa. Lebanon lazima ipinge shinikizo la Marekani la kupokonywa silaha Harakati ya Mapambano ya Kiislamuu ya Hizbullah ya Lebanon.

Huku kukiwa na ongezeko la ghasia na ukandamizaji wa Israel unaombatana na mauaji ya kimbari huko Gaza, kiongozi huyo wa Palestina amelaani ukandamizaji wa vyombo vya habari na kuonya juu ya upanuzi wa Wazayuni, akiangazia hali mbaya zaidi ya kibinadamu.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, mashirika ya kimataifa ya misaada na haki za binadamu pia yameripoti juu ya kuendelea kuzuia utawala wa Kizayuni mchakato wa misaada ya kuingia Ukanda wa Gaza, mashambulizi ya makusudi ya utawala huo dhidi ya vikosi vinavyotoa usalama kwa misafara ya misaada, na kuuawa shahidi Wapalestina wasiopungua 1,769 kwa kupigwa risasi na jeshi la Kizayuni wa Israel walipokuwa wakisubiri kupokea misaada.