-
Gaza inahusiana vipi na janga la Srebrenica?
Jul 12, 2025 06:11Katika mwaka wa 30 wa kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya Srebrenica, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika katika ujumbe wake akisema: "Lau dunia ingejifunza kutokana na janga hilo, tusingeshuhudia mauaji mengine ya kimbari dhidi ya Waislamu hii leo, na mara hii huko Gaza."
-
Uhispania na Ireland kujiunga na nchi zaidi ya 20 zitakazochukua 'hatua madhubuti' dhidi ya Israel
Jul 11, 2025 13:15Uhispania na Ireland zitajiunga na zaidi ya nchi 20 zitazokutana katika mji mkuu wa Colombia, Bogota wiki ijayo kutangaza "hatua madhubuti" dhidi ya ukiukaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel.
-
IAEA: Baada ya miezi michache, Ujerumani itaweza kuunda silaha za nyuklia
Jul 11, 2025 10:39Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati IAEA Rafael Grossi ametangaza kuwa, Ujerumani inaweza kutengeneza silaha zake za nyuklia ndani ya kipindi cha miezi kadhaa ikiwa itachagua kufanya hivyo. Katika mahojiano na tovuti ya habari ya Poland ya Reczpospolita Grossi amesema Berlin tayari ina nyenzo muhimu za nyuklia, ujuzi na ufikiaji wa teknolojia ya kuunda silaha hizo.
-
Kuhusu vikwazo vya Trump dhidi yake, Albanese asema mwiba wake ‘umechoma ndipo’
Jul 11, 2025 10:14Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina, Francesca Albanese, amesema hakatishwi tamaa na vikwazo alivyowekewa na Marekani. "Inaonekana mwiba umechoma ndipo," amesema Bi Albanese katika kipindi cha mubashara cha televisheni.
-
Jibu la swali la leo; Kwa nini Ujerumani inataka kuongeza kwa kiasi kikubwa gharama zake za kijeshi?
Jul 11, 2025 04:48Katika hotuba yake kwa bunge la nchi hiyo Bundestag, Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, sambamba na kuunga mkono ongezeko kubwa la gharama na matumizi ya kijeshi, alisisitiza kuwa anataka kuligeuza jeshi la nchi yake kuwa taasisi ya kupigiwa mfano na inayoongoza katika Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO).
-
'Mauaji ya kimbari Gaza ni matokeo ya dunia kushindwa kujifunza kutoka mauaji ya Srebrenica'
Jul 11, 2025 04:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa iwapo dunia ingezingatia kikamilifu mafunzo kutoka mauaji ya kimbari ya Srebrenica huko Bosnia, basi leo hii tusingeshuhudia jinai nyingine dhidi ya Waislamu, kama inavyotokea Gaza.
-
Unajua kwa nini Marekani imemuwekea vikwazo Ripota Maalumu wa UN kuhusu Maeneo ya Palestina Yanayokaliwa kwa Mabavu?
Jul 10, 2025 22:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alitangaza Jumatano, Julai 9, kwamba atamuwekea vikwazo Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Maeneo ya Palestina Yanayokaliwa kwa Mabavu, kwa kile alichokiita "juhudi zisizo halali zinazohusiana na uchunguzi wake kuhusu vita vya Israel dhidi ya watu wa Gaza" na eti kwa kuchukua "hatua dhidi ya maafisa wa Marekani na Israel."
-
US yamwekea vikwazo ripota wa UN Albanese kwa kukosoa jinai za Ghaza
Jul 10, 2025 02:49Marekani imetangaza kuwa inamwekea vikwazo ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Palestina, Francesca Albanese.
-
Borrell amkemea Netanyahu kwa kutaka Trump apewe Tuzo ya Amani ya Nobel
Jul 10, 2025 02:39Mkuu wa zamani wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amekemea pendekezo la waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu la kutaka rais wa Marekani Donald Trump atunukiwe Tuzo ya Amani ya Nobel, akilielezea hilo kuwa ni hatua iliyochukuliwa na "mtu anayeaminika kuwa mhalifu wa kivita" kwa ajili ya "muuzaji wake mkuu wa silaha".
-
Kwa nini watu wengi duniani wana mtazamo hasi kuhusu Marekani?
Jul 09, 2025 23:19Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliochapishwa na Kituo cha Utafiti cha Pew, watu wa Canada na Mexico, majirani wawili wa karibu wa Marekani, wanaitambua nchi hiyo kuwa tishio kubwa zaidi kwao.