-
Trump aitishia EU kwa ushuru wa forodha wa 50%
May 24, 2025 03:21Rais wa Marekani Donald Trump amependekeza "ushuru wa moja kwa moja wa 50%" kwa nchi zote za Umoja wa Ulaya, akitaja nakisi ya biashara ya dola milioni 250 kila mwaka na umoja huo. Amependekeza kuwa kiwango hicho kipya cha ushuru kianze kutekelezwa Juni 1.
-
Mbunge wa US ataka Gaza iangamizwe kwa nyuklia kama Hiroshima
May 23, 2025 08:25Mbunge wa jimbo la Florida wa chama cha Republican, Randy Fine ameashiria shambulio la bomu la nyuklia la Marekani dhidi ya Japan wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na kutoa wito wa kuangamizwa Gaza kwa silaha za nyuklia.
-
Umoja wa Ulaya kutazama upya mkataba wa ushirikiano wake na Israel
May 22, 2025 23:10Kufuatia kushadidi jinai za utawala wa kibaguzi wa Israel huko Gaza na kuibuliwa mzozo wa kibinadamu usio na mfano wake katika ukanda huo unaozingirwa, Umoja wa Ulaya umeanza kufanyia marekebisho makubwa mapatano ya biashara na ushirikiano kati yake na Israel.
-
Wafanyakazi wawili wa ubalozi wa Israel wauawa kwa kupigwa risasi Washington
May 22, 2025 09:06Wafanyakazi wawili wa ubalozi wa utawala haramu wa Israel mjini Washington wameuawa kwa kupigwa risasi jana jioni, nje ya Jumba la Makumbusho la Kiyahudi katika mji mkuu wa Marekani. Hayo ni kwa mujibu wa maafisa na vyombo vya habari.
-
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu mpango hatari wa Israel dhidi ya watu wa Gaza
May 22, 2025 08:59Umoja wa Mataifa umetoa taarifa na kuonya kwamba mpango mpya wa Israel wa kusambaza misaada huko Gaza umekuwa chombo cha ulaghai na kuwahamisha wakazi wa eneo hilo, na ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu.
-
Kwa nini Marekani inafuatilia suala la kuongeza bajeti za kijeshi za wanachama wa NATO?
May 22, 2025 03:17Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kufikia mkutano wa kilele wa NATO mwezi Juni mwaka huu, nchi zote wanachama wa muungano huo wa kijeshi zitakuwa zimekubaliana kutenga asilimia 5 ya pato lao la ndani kwa ajili ya ulinzi katika kipindi cha muongo mmoja ujao.
-
ASEAN kufanya mikutano kuhusu Myanmar
May 21, 2025 23:01Jumuiya ya mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN inatarajia kuiitisha mikutano miwili mahsusi kwa ajili ya kkujadili hali ya mambo nchini Myanmar.
-
Sababu za kukatisha tamaa mazungumzo ya simu ya Trump na Putin kuhusu usitishaji vita nchini Ukraine
May 21, 2025 07:49Kuakisiwa mazungumzo ya simu kati ya Donald Trump na Putin kunaonyesha mfadhaiko na kutiliwa shaka kubwa juhudi za kumaliza vita nchini Ukraine.
-
Demokrasia ya BBC; "Uhuru wa kujieleza" ni kwa wapinzani wa Iran tu!
May 21, 2025 03:25Gary Lineker, mtangazaji mashuhuri na maarufu wa BBC, amefutwa kazi na shirika hilo baada ya miaka 26 ya utumishi kwa sababu tu ya kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
"Msingi wa uhusiano wa Russia, Afrika ni mshikamano wa zama za Sovieti"
May 20, 2025 22:56Russia imesema serikali nyingi za Kiafrika zimedumisha msimamo huru, uliojikita katika kutoingilia kati masuala ya nchi nyingine, kuheshimu mamlaka ya kujitawala na uhuru wa kitaifa, na zimekataa kupasisha vikwazo dhidi ya Russia licha ya mashinikizo makubwa kutoka kwa nchi za Magharibi.