-
Russia kushirikiana na US kwenye faili la nyuklia la Iran
Mar 10, 2025 07:54Russia imeeleza nia ya kushirikiana na Marekani katika kushughulikia masuala ya Asia Magharibi, ikiwa ni pamoja na mradi wa nyuklia wa Iran, ikizingatiwa kuwa uhusiano wa Moscow na Washington unazidi kuimarika.
-
Pyongyang yajibu mapigo, yavurumisha makombora baharini
Mar 10, 2025 07:52Korea Kaskazini imevurumisha makombora kadhaa ya balestiki baharini leo Jumatatu, saa chache baada ya wanajeshi wa Korea Kusini na Marekani kuanza mazoezi makubwa ya kijeshi ya kila mwaka ya pamoja, ambayo Pyongyang inayatazama kama majaribio ya uvamizi.
-
Ripota Maalumu wa UN: Vitendo vya Israel katika Ukingo wa Magharibi ni aibu na kinyume cha sheria
Mar 09, 2025 23:00Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa amevitaja vitendo vya utawala wa Kizayuni katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kuwa ni vya fedheha na kinyume cha sheria.
-
Beijing: Majeshi ya Iran, Russia, China kufanya mazoezi ya pamoja ya majini
Mar 09, 2025 22:59Mazoezi ya pamoja ya majeshi ya majini yatakayohusisha vikosi vya wanamaji vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia na China yamepangwa kufanyika katika eneo la kaskazini mwa bahari ya Hindi, ambapo mataifa hayo matatu yatashiriki katika operesheni kubwa za baharini zinazojumuisha vitengo mbalimbali vya vikosi vyao vya jeshi.
-
Wafaransa, Wajerumani na Waingereza wanamtambua Trump kuwa ni dikteta
Mar 09, 2025 22:58Utafiti mpya unaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya Wafaransa, Wajerumani na Waingereza wanamtambua Rais wa Marekani, Donald Trump, kuwa ni dikteta.
-
The Guardian: Trump anajifanya tu mbabe lakini ni mtu dhaifu
Mar 09, 2025 07:53Gazerti la The Guardian la nchini Uingereza limeandika makala maalumu kuhusu misimamo dhaifu ya rais wa Marekani, Donald Trump katika masuala tofauti na kusema kuwa, ijapokuwa rais huyo anajifanya mbabe, lakini ni mtu dhaifu na vitisho vyake havina maana.
-
Wainjilisti wamshinikiza Trump kulipa wema, wamtaka aruhusu kunyakuliwa Ukingo wa Magharibi
Mar 09, 2025 07:52Ripoti iliyochapishwa katika gazeti la Marekani, The New York Times, imefichua kwamba Wakristo wa Kiinjilisti, ambao walitoa huduma kubwa kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, wakati wa uchaguzi uliopita, ambapo karibu asilimia 80 walimpigia kura, sasa wanasubiri alipe fadhila na kuiruhusu Israel kutwaa Ukingo wa Magharibi, kwa madai ya ahadi ambayo eti Mungu aliwaahidi Wayahudi katika Biblia.
-
UN: Utawala wa Trump uache kuingilia uhuru wa mahakama
Mar 08, 2025 23:08Ripoti Maalumu wa Umoja wa Mataifa amekosoa vikali hatua za hivi majuzi za serikali ya Donald Trump ya kuwatimua na kuwateua maafisa wapya wa mahakama, akielezea wasiwasi wake kwamba hatua hizi ni sehemu ya vitisho kwa uhuru wa mfumo wa mahakama wa Marekani.
-
Korea Kaskazini: Tutatoa jibu kali kwa maneva ya kijeshi ya Korea Kusini na Marekani
Mar 08, 2025 23:06Korea Kaskazini imeionya Seoul na kutishia kuchukua hatua kali iwapo mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya kila mwaka kati ya Korea Kusini na Marekani yataendelea katika wiki zijazo.
-
Wacanada wenye hasira wamjibu kivitendo Donald Trump
Mar 08, 2025 23:06sambamba na hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump, ya kuongeza mashinikizo kwa Ottawa nwa vitisho vyake vya kuiteka Canada na kuijumuisha kwenye majimbo ya Marekani, wananchi wenye hasira wa Canada nao wameamua kutokaa kimya na wameanza kwa nguvu kutekeleza vikwazo dhidi ya bidhaa za Marekani.