Wafaransa, Wajerumani na Waingereza wanamtambua Trump kuwa ni dikteta
https://parstoday.ir/sw/news/world-i123700-wafaransa_wajerumani_na_waingereza_wanamtambua_trump_kuwa_ni_dikteta
Utafiti mpya unaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya Wafaransa, Wajerumani na Waingereza wanamtambua Rais wa Marekani, Donald Trump, kuwa ni dikteta.
(last modified 2025-03-09T22:58:56+00:00 )
Mar 09, 2025 22:58 UTC
  • Wafaransa, Wajerumani na Waingereza wanamtambua Trump kuwa ni dikteta

Utafiti mpya unaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya Wafaransa, Wajerumani na Waingereza wanamtambua Rais wa Marekani, Donald Trump, kuwa ni dikteta.

Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya "Common Destiny", 59% ya Wafaransa na Wajerumani, 56% ya Waingereza na 47% ya Wapolandi wanamtambua Rais wa Marekani, Donald Trump kuwa ni dikteta.

Matokeo ya kura hiyo ya maoni yametolewa huku Ukraine ikiendelea kuandamwa vikali na Donald Trump. Katika siku za hivi karibuni pia Washington imekata misaada ya kijeshi na upelelezi kwa Ukraine. Kinyume chake, nchi za Ulaya zinafanya jitihada za kufidia kupunguzwa kwa misaada ya Marekani kwa Ukraine na kuanzisha nguvu ya ulinzi katika bara hilo, juhudi ambazo hadi sasa hazijafanikiwa.

Uchunguzi huo wa maoni umebaini kuwa, robo ya watu wa Ufaransa tu ndio wanaoiona Marekani kama "mshirika" wao. 

Vilevile Wafaransa 8 kati ya 10 (76%) wanasema wana wasiwasi mkubwa kuhusu kupanuka migogoro barani Ulaya katika miaka ijayo.