-
Waziri Mkuu wa Uhispania: Sitaruhusu mpango wa Trump wa kuwafukuza Wapalestina huko Gaza
Feb 16, 2025 10:23Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez, amepinga vikali mpango wa Rais wa Marekani wa kutwaa Ukanda wa Gaza na kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina hadi nchi jirani kama Jordan na Misri, akisisitiza kwamba Madrid haitaruhusu mpango huo kutekelezwa.
-
Kadi nyekundu yatolewa kwa Israel kwenye mechi kati ya Osasuna na Real Madrid
Feb 16, 2025 05:56Mashabiki wa klabu ya Osasuna ya Uhispania wametoa wito wa kukomeshwa uhalifu wa utawala wa Israel huko Palestina katika mechi na mpira wa miguu iliyofanyika jana Jumamosi kati ya timu hiyo dhidi ya Real Madrid.
-
NBC: Trump amtaka Zelensky ampatie umiliki wa asilimia 50 wa madini adimu ya Ukraine
Feb 16, 2025 04:29Kwa mujibu wa maafisa wanne wa Marekani, utawala wa Trump umependekeza kwa Ukraine kwamba iwapo nchi hiyo itaipatia Marekani asilimia 50 ya madini yake adimu, iko tayari kutuma wanajeshi wake ili kuilinda Ukraine iwapo itafikia makubaliano na Russia.
-
Kellogg: Marekani inataka 'kuvunja' muungano wa Russia na Iran
Feb 16, 2025 04:24Keith Kellogg Mjumbe maalumu wa Washington kwa ajili ya Ukraine na Russia amesema kuwa Marekani inataka kuvunja muungano uliopo kati ya Russia, Iran na China.
-
UN yalaani mashambulizi ya Israel katika Ukingo wa Magharibi
Feb 16, 2025 04:22Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) imelaani mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Israel katika eneo la Ukingo wa Magharibi na kuutaka utawala huo kusitisha mara moja "wimbi la tahadhari ya machafuko na ukimbizi wa umati'' kwa raia wa Palestina.
-
UNICEF: Intaneti inafaidisha watoto lakini kuna hatari
Feb 15, 2025 08:48Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limesema, maisha ya watoto na vijana kwa muda mrefu yameunganishwa na intaneti na mitandao ya kijamii na kadri teknolojia inavyoendelea kubadilika kwa kasi jambo hili linaongezeka na kuenea zaidi na kuruhusu watoto kufikia ulimwengu wa habari, kujifunza, kushirikiana, burudani na zaidi inaweza kuwa chanya lakini wakati mwingine kuna hatari.
-
Mahathir azikosoa EU, US kwa mauaji ya kimbari Gaza, asema 'Ustaarabu umefeli'
Feb 15, 2025 03:46Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia amekosoa vikali uungaji mkono wa Marekani na Umoja wa Ulaya kwa Israel akisisitiza kuwa, kuunga mkono kwa hali na mali mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza ni jambo la 'kuchukiza na kukirihisha.'
-
Mtaalamu wa Zambia: Ushuru wa Trump utawadhuru zaidi Wamarekani
Feb 14, 2025 23:12Mtaalamu mmoja wa masuala ya biashara, ujasiriamali na uwezekaji wa Zambia amesema uamuzi wa serikali ya Marekani wa kutoza ushuru wa juu kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Canada, Mexico, na China utawadhuru zaidi Wamarekani.
-
Balozi wa UN aionya US kuiweka Ansarullah kwenye orodha ya magaidi
Feb 14, 2025 08:38Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen, Hans Grundberg ameonya kuhusu athari mbaya za Marekani kuitambua Harakati ya Ansarullah ya Yemen kuwa kundi la kigeni la kigaidi, kutokana na mashambulizi ya kundi hilo la Muqawama ya kulipiza kisasi dhidi ya maeneo ya Israel.
-
Wabunge wa Marekani, makuhani nao wapinga mpango wa Trump wa kutwaa Gaza
Feb 14, 2025 04:38Mamia ya wabunge na makuhani wa Kiyahudi wa Marekani wametangaza upinzani wao dhidi ya mpango wa Rais Donald Trump wa kutaka kuliitwaa eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina na kuwahamisha kwa mabavu wakazi wake.