UNICEF: Intaneti inafaidisha watoto lakini kuna hatari
https://parstoday.ir/sw/news/world-i122774-unicef_intaneti_inafaidisha_watoto_lakini_kuna_hatari
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limesema, maisha ya watoto na vijana kwa muda mrefu yameunganishwa na intaneti na mitandao ya kijamii na kadri teknolojia inavyoendelea kubadilika kwa kasi jambo hili linaongezeka na kuenea zaidi na kuruhusu watoto kufikia ulimwengu wa habari, kujifunza, kushirikiana, burudani na zaidi inaweza kuwa chanya lakini wakati mwingine kuna hatari.
(last modified 2025-02-15T08:48:10+00:00 )
Feb 15, 2025 08:48 UTC
  • UNICEF: Intaneti inafaidisha watoto lakini kuna hatari

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limesema, maisha ya watoto na vijana kwa muda mrefu yameunganishwa na intaneti na mitandao ya kijamii na kadri teknolojia inavyoendelea kubadilika kwa kasi jambo hili linaongezeka na kuenea zaidi na kuruhusu watoto kufikia ulimwengu wa habari, kujifunza, kushirikiana, burudani na zaidi inaweza kuwa chanya lakini wakati mwingine kuna hatari.

UNICEF inaeleza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, kuna dhana potofu nyingi ambazo zimeenea kuhusu athari za teknolojia za kidijitali kwenye maisha ya watoto, na kuwapotosha wazazi, walezi, waelimishaji na watunga sera.

Kwa msingi huo UNICE imesema  mwaka huu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtandao Salama, kuna haja ya kuzingatia baadhi ya dhana hizo potofu.

UNICEF imesema  wakati watoto wananufaika kwa kutumia muda wao mtandaoni, na wakati usawa katika ufikiaji ni lengo la msingi, ufikiaji mkubwa pia mara nyingi hushuhudia watotowakiwa hatarini kukumbana na ujumbe wa chuki na picha za vurugu mtandaoni.

Ingawa intaneti inaweza kuchochea muunganisho wa kijamii, ushiriki na ubunifu kwa watoto, lakini kwa kuwa mazingira yao ya kidijitali bado hayadhibitiwi, na mara chache hayabuniwi kwa kuzingatia maslahi yao bora, pia hurahisisha kuenea kwa maudhui hatari kama vile jumbe za chuki na picha za kutatanisha.

UNICEF imesema serikali zinapaswa kutunga será thabiti ili wahusika walazimike kujumuisha uzingatiaji wa haki za watoto, ikijumuisha tathmini thabiti za athari, katika mchakato wa kudhibiti chuki na vurugu mtandaoni.