-
Amnesty: Hatua ya Marekani ya kumkaribisha Netanyahu ni kudharau haki na uadilifu wa kimataifa
Feb 05, 2025 03:29Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limelaani kitendo cha Marekani cha kumpokea waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu.
-
Trump atamka rasmi: Marekani itawahamisha Wapalestina na 'itaitwaa' na 'kuimiliki' Ghaza
Feb 05, 2025 02:22Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza hadharani kwamba Marekani itachukua udhibiti wa Ukanda wa Ghaza, na kulijenga upya eneo hilo lililoharibiwa na vita na kuandaa fursa za kiuchumi kwa wakazi wake wa baadaye; na alipoulizwa kama atapeleka huko wanajeshi wa Marekani, Trump ameapa "kufanya kitakacholazimu."
-
Lavrov: Sera ya 'Marekani Kwanza' inatoa mwangwi wa kaulimbiu ya Hitler ya 'Ujerumani iko juu ya wote'
Feb 05, 2025 02:21Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov ametahadharisha kuwa, sera ya Trump ya ‘Marekani Kwanza’ ina mfanano wa kutatanisha na kaulimbiu ‘Ujerumani iko juu ya wote’ iliyotumiwa na Wanazi kuthibitisha ukuu na kuwa bora kitaifa kuliko wengine.
-
Kwa nini mataifa ya Ulaya yanaunga mkono chuki dhidi Uislamu?
Feb 04, 2025 23:09Ikiwa ni katika muendelezo wa siasa za chuki dhidi ya Uislamu mwanasiasa mwenye uraia pacha wa Sweden na Denmark na mwenye chuki dhidi ya Uislamu, Rasmus Paludan kwa mara nyingine tena ameivunjia heshima Qur'ani Tukufu kwa kuchoma moto nakala ya kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu katika mji mkuu wa Denmark, Copenhagen.
-
WHO yajibu tuhuma za US: Hatuegemei upande wa nchi yoyote mwanachama, tunazingatia sayansi
Feb 04, 2025 07:02Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesisitiza kuwa shirika hilo haliegemei upande wa nchi yoyote mwanachama na kwamba limeanzishwa kwa ajili ya kuhudumia nchi zote na watu wote.
-
Shirika la Ujasusi la Russia: NATO inapanga kumuondoa madarakani rais wa Ukraine, Zelensky
Feb 04, 2025 06:58Shirika la kijeshi la NATO linafikiria kufanikisha mpango wa kumuondoa madarakani Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky kwa 'kumchafua' kabla ya uchaguzi ujao utakaofanyika mwakani. Hayo yameelezwa katika ripoti iliyotolewa na Shirika la Ujasusi la Russia la Nje ya Nchi (SVR).
-
Jimbo la Ontario Canada laziwekea vikwazo kampuni za Marekani
Feb 03, 2025 23:18Baada ya Donald Trump kuiambia Canada kuwa atatoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za nchi hiyo zinazoingia Marekani, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amejibu kivitendo hatua hiyo akitangaza kuwa bidhaa za Marekani zinazoingia nchini humo nazo zitatozwa ushuru wa asilimia 25.
-
Vipi Canada na Mexico zimeingia katika vita vya kibiashara na Marekani?
Feb 03, 2025 22:54Baada ya Rais Donald Trump kuanzisha vita vya kibiashara dhidi ya Canada na Mexico kwa kuweka ushuru wa 25% kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka katika nchi hizo, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ametangaza ushuru wa 25% kwa bidhaa zilizoagizwa kutoka Merika kama hatua ya kulipiza kisasi.
-
Vita baina ya Marekani na Canada sasa vyaingia michezoni; wimbo wa taifa wa Marekani wazomewa
Feb 03, 2025 07:01Mashabiki wa michezo wa Canada wamekuwa wakizomea wimbo wa taifa wa Marekani kila unapopigwa katika mechi mbalimbali ikiwa ni kuonesha hasira zao kwa amri ya rais wa Marekani Donald Trump ya kutozwa ushuru mkubwa bidhaa zinazoingizwa Marekani kutokea Canada.
-
Rais wa Russia: Karibuni hivi viongozi wote wa Ulaya 'watamtikisia mikia' Trump japo hawampendi
Feb 03, 2025 02:23Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, Umoja wa Ulaya daima umekuwa ukipokea ishara za uchukuaji hatua zake za kisiasa kutoka Washington na utaendelea kufanya hivyo wakati huu Donald Trump akiwa madarakani; na kwamba licha ya baadhi ya viongozi wa umoja huo kupinga vikali kuchaguliwa tena Trump, rais huyo mpya wa Marekani "atarejesha utulivu" na utiifu wa EU "haraka sana".