Jimbo la Ontario Canada laziwekea vikwazo kampuni za Marekani
-
Doug Ford
Baada ya Donald Trump kuiambia Canada kuwa atatoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za nchi hiyo zinazoingia Marekani, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amejibu kivitendo hatua hiyo akitangaza kuwa bidhaa za Marekani zinazoingia nchini humo nazo zitatozwa ushuru wa asilimia 25.
Sasa kiongozi wa Ontario, jimbo lenye watu wengi zaidi huko Canada ambalo linaunda takriban asilimia 38 ya pato la taifa pia limeweka wazi baadhi ya matokeo ya hatua za Trump kwa makampuni ya Marekani yanayofanya kazi katika jimbo hilo. Doug Ford amesema kuwa makampuni ya Marekani yatapigwa marufuku mara moja kutoka kwa kandarasi za jimbo la Onario hadi hapo Marekani itakapondoa ushuru wake ulioainisha kwa Canada.
Ford amesema, wafanyabiashara wa Marekani watarajie kupoteza makumi ya mabilioni ya dola katika mapato mapya,na wanapasa kumlaumu Rais Trump kwa hatua yake hii.
Mkuu wa jimbo la Ontario ameendelea kubainisha kuwa jimbo hilo litachukua hatua zake mkabala wa hatua za Rais Trump ambayo Ontario kusimamisha kandarasi iliyosainiwa mwezi Novemba mwaka jana kati ya jimbo hilo na kampuni ya satelaiti ya Elon Musk ya Starlink, kampuni inayotoa huduma ya mtandao wa kasi duniani kote.
Amesema, Musk ni mmoja wa washirika wa karibu wa Trump, na kama mhariri wao wa uchumi anavyoeleza, uamuzi huu unaweza kuwa ulifanywa kwa matumaini ya kuwalazimisha wasaidizi wa Trump kukabiliana na Rais kuhusu gharama ya sera zake.